Benny Kisaka |
Na Mahmoud
Zubeiry
MWENYEKITI
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Abbas Pinto
amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwakilishi wa Klabu katika uchgauzi wa
Chama cha Soka Dar es Salaam.
Juma Pinto |
Winga huyo
wa timu ya mkoa wa Dar es Salaam, Mzizima United iliyoshiriki Kombe la Taifa,
Taifa Cup mwaka 1997 mkoani Kagera, kwa kuchukua fomu ya kuomba nafasi hiyo, ina
maana atachuana na Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Concepts Limited, Benny
Kisaka, ambaye pia ni Mwana Habari.
Wagombea
wengine katika nafasi hiyo ni Philemon Ntahilaja na Frank Mchaki, wakati
wanaowania Ujumbe wa Mkutano Mkuu ni Isaac Mazule, Shufaa Jumanne, Shaffi Dauda
na Muhisn Balhabou, huku Shaaban Mohamed, Andrew Tupa, Siza Abdallah Chenje,
Sunday Mwanahewa, George Wakuganda na Lameck Nyambaya wakiwania Ujumbe wa Kamati
ya Utendaji.
Wanaowania
Uenyekiti ni Ahmad Seif Hemed ambaye anachuana na Brown Ernest, Salum Mkemi,
Evans Aveva, Ayoub Nyenzi, Juma Jabir na Meba Ramadhan, wakati nafasi ya Makamu
Mwenyekiti ni Ally Mayay na Salum Mwaking’inda, na Ukatibu Mkuu, Said Tuliy na
Hamisi Ambari ndio waliojiotokeza hadi sasa, ingawa kuna habari Rahim Kangezi
‘Zamunda’ naye atachukau fomu.
Uchaguzi wa
DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za kugombea nafasi mbalimbali
zilianza kutolewa tangu Oktoba 29, wakati Novemba 4 hadi 8, Kamati ya Uchaguzi,
chini ya Mwenyekiti wake, Juma Simba itapitia fomu za walioomba
uongozi.
Novemba 9
hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea, ambazo zitajadiliwa Novemba 14
hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa ya kukata rufaa, ambazo
zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo, Novemba 25 yatatangazwa
majina ya wagombea waliopitishwa.
Uchaguzi wa
DRFA utafanyika siku chache tu kabla ya uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), mwishoni mwa Desemba, mwaka huu.Kwa hisani ya Bin Zubeiry
Blog
Post a Comment