MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Simon Mwapagata ‘Kapturado’ amewashauri wasanii walioingia katika tasnia ya filamu wakitokea katika tasnia ya ulimbwende warudi huko baada wao kuwa ni chanzo cha kashifa katika tasnia ya filamu Bongo Rado anasema kuwa walimbende hao ndio wanaovuma kwa matukio ngono na mavazi ya kujifedhehesha.
“Mimi nikiwa kama
mwanzilishi ya Bongo Movie Unity nina uchungu sana na tabia ya hawa akina dada
waliovamia tasnia ya filamu wakitokea katika fani ya urembo wamekuja kutuharibia
tasnia ya filamu kwa kufanya matukio ya ajabu ajabu, ngono mara mavazi ya nusu
uchi hiyo siyo filamu ninawashauri warudi kwa Lundenga ndio anawezana
nao,”anasema Rado kwa uchungu.
Rado amedai kuwa sababu
kubwa ya kuanzishwa kwa kundi hilo ililenga kubororesha tasnia ya filamu na si
sehemu ya baadhi ya wasanii kuja kujiuza au kuvaa nusu uchi katika majukwaa kama
ambavyo imekuwa ikifanyika madongo yaliwalenga wasanii ambao ambao ni gumzo kwa
kashifa Bongo Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ambao wote waliingia katika tasnia ya
filamu wakitokea umiss.
Chanzo: habari hii ni
kwa hisani ya www.filamucentral.co.tz


Post a Comment