Kalusha Mbwalya Rais wa
Shirikisho la soka Zambia FAZ, katikati ni Balozi wa Tanzania nchini zambia
Grace Mujuma na kulia ni afisa balozi wa Tanzania nchini Zambia Jeswald
Majuva wakiwa katika picha ya pamoja.
Pichani kulia ni Rais wa
Shirikisho la soka Zambia FAZ,Kalusha Bwalya akiwa ofisini kwa Balozi wa
Tanzania nchini humo,kwa ajili ya uthibitisho wa kutoa taarifa ya ujio wa timu
ya Taifa ya Zambia Chipolo polo nchini Tanzani kwa ajili ya kucheza na timu ya
Tanzani ,aidha imeelezwa kuwa timu ya Chipolo polo itainigia nchini Desemba 16
na kukaa takribani wiki nzima nchini Tanzania kwa kufanya mafunzo yao ya
maandalizi ya kwenda Afrika Kusini.Habari kwa hisani ya Mdua wa Jiachie Blog
aliyeko Zambia.
======== =======
========
Rais wa Shirikisho la
Soka Zambia FAZ Bwana Kalusha Mbwalya amesema Timu ya soka ya Taifa ya
Zambia wanaafrican champion wanachipolopolo wanatarajia kucheza mechi ya
kirafiki na Timu ya Taifa ya Tanzania , Taifa Stars katika uwanja wa Taifa
jijini DSM .
‘ hivi sasa tumeshakubaliana na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF kuhusu mechi hii ya kirafiki ambayo inatarajia kuchezwa tarehe 22 mwezi Desemba “
Taarifa hii iemtolewa mjini Lusaka Zambia katika Ofisi za ubalozi wa Tanzania wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Grace Mujuma.
Rais wa FAZ , amesema katika mechi hiyo ya kirafiki wa nampango pia wa kushirikisha kikosi kizima cha wachezaji wa timu ya wanachipolopolo kwa lengo la kuifanya mechi hiyo iwe nzuri zaidi.
“Tuna mpango wa kushirikisha kikosi kizma cha wachezaji wanaocheza ndani ya nchi ya Zambia na hali kadhalika wachezaji ia wanochezea katika timu mbalimbali nje ya nchi , huu ndio mkakati wetu kabambe katika maandalizi ya michuano yanayokuja nchini Afrika ya Kusini” alisema Kalusha
Aidha amefafanua kuwa katika mechi hii ya kirafiki kati ya Zambia na Tanzania wameona pia waweke kambi maalum ya amfunzo ya wiki nzima nchini Tanzania kwa lengo la kujiandaa na michuano inayotarajia kufanyika nchini Afrika ya Kusini mwakani .
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Zambia Grace Mujuma amesema kufanyika kwa mechi hiyo ya kirafiki nchini Tanzania itakuwa ndio nafasi ya kujipima zaidi kwa wachezaji wa Taifa Stars .
“Mchezo huu utakuwa chachu kubwa kwa wachezaji wa Tanzania kujipima na hali kadhalika kujifunza zaidi kwa wachezaji hawa wa soka wa Zambia jinsi gani wanavyocheza mpira wa soka’ alisema Balozi Mujuma
Mujuma pia amewataka watanzania mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuona mechi hiyo itakayokuwa ya mfano wake nchini Tanzania, kutokana na timu hiyo ya Zambia hivi sasa imejipatia umaarufu mkubwa wa kushinda michuano ya AFCON 2012 .
Timu hiyo ya soka ya Zambia imepanga kusafiri tarehe 16 kutoka mjini Lusaka Zambia na ndege ya Precision Airways kuelekea jijini DSM kushiriki mechi hiyo ya kirafiki inayotarajia kuchezwa tarehe 22 mwezi DESEMBA katika uwanja wa kimataifa wa mpira wa soka jijini DSM.

Post a Comment