Kaseja kulia akizungumza na kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen hivi karibuni |
Na Bin
Zubeiry
NAHODHA wa
Simba, Juma Kaseja amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia yeye na klabu hiyo
basi.
BIN ZUBEIRY amefika kwenye mazoezi ya Simba jioni ya leo Uwanja
wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam na kukuta wachezaji wote wakiendelea na
mazoezi kujiandaa na mechi ya Toto African mwishoni mwa wiki, kasoro Kaseja na
Amir Maftah.
Alipoulizwa
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kwamba Maftah ana ruhusa maalum
kwa sababu ameoa hivi karibuni, lakini Kaseja hawana taarifa zake, ila; “Nadhani
hatakuwa vizuri kisaikolojia baada ya kufanyiwa fujo Jumamosi,”alisema
Kamwaga.
Lakini
BIN ZUBEIRY ilipozungumza na wachezaji wenzake, walisema Nahodha
wao amewaaga kwamba yeye na Simba basi, kwani ameumia sana kwa jinsi
alivyodhalilishwa na mashabiki Jumamosi Morogoro.
“Juma hapa
ndio basi kaka, Kasema yeye na Simba basi, amesononeshwa mno na jinsi
alivyodhalilishwa baada ya mechi ya Morogoro,”alisema mchezaji mmoja wa Simba
baada ya mazoezi Kinesi leo.
Kaseja
alitukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba baada ya mechi dhidi ya
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya
kizembe.
Lakini
tayari uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho alivyotolewa kipa wao
huyo namba moja, na kusema wanafikiria kuwachukulia hatua kali watu
waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo.
Juhudi za
kumpata Kaseja mwenyewe kuzungumzia suala hilo, hazikuweza kufanikiwa kwani simu
yake ilikuwa haipatikani.
Post a Comment