Watanzania wajumuika kwa
wingi katika mkutano wa Worldmission Sunday uliofanyika jumapili ya tarehe
28.10.12. watanzania hao ambao walitoka pande mbali mbali za ujerumani,
walihudhuria mkutano huo ambao ulianza saa nne asubuhi mpaka saa 6 za mchana.
baada ya chakula cha mchana mkutano huo uliendelea hadi saa 12 za
jioni.
Dr, Isak Majura
alitambulisha Taifa la Tanzania kwa kuonyesha Presentation ambayo ilitayarishwa
na Jumuiya ya Watanzania Ujerumani (UTU)
Vile vile Katibu wa U T
U alionyesha Presentation ya mradi wa shule ya msingi ya iliyopo maeneo ya
Kigamboni Dar Es Salaam. ambapo wafadhili kadhaa walionyesha kushawishika sana
na kutaka kujua ni jinsi gani wanaweza kuifikia shule hiyo ili kuangalia
uwezekano wa kuchangia chochote katika maendeleo ya shule
hiyo.
Mara baada ya kukamilika
kwa presentation hizo Mgeni Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani
Bw. Ali Siwa allitoa salam Rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania na kuwashukuru
watayarishaji wa Mkutano huo kwa upendo na mualiko kwa Umoja wa Watanzania
Ujerumani.
Wakati huo huo Bi Tabia
Mwanjelwa, (Muimbaji wa Maquiz wa Zamani) aliburudisha kwa kuimba na kupiga
gitaa, ambapo aliwaacha hoi wafadhili waliohudhuria katika mkutano huo, Bi Tabia
Mwanjelwa alisema sauti yake na utaalamu wake wa kupiga Gitaa ndio mchango wake
kwa Watanzania.
Watayarishaji wa
Mkutano huo wamefurahishwa na wameridhika sana na mahudhurio ya Watanzania,
pamoja na presentation zote mbili, na kuahidi kuwa Umoja wa watanzania
Ujerumani watapata mialiko mara kwa mara kunapotokea hafla za aina
hii.
Umoja ni Nguvu
!
kamati.utu@googlemail.com
Post a Comment