MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha leo kesi inayomkabili msanii wa filamu Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28) baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hata hivyo,
wakili wa utetezi Peter Kibatala aliomba
mahakama kuhimiza upande wa mashtaka kuongeza kasi ya upelelezi kwa kuwa
mshtakiwa anateseka mahabusu.
Hakimu Mkazi
Augustina Mmbando alisema upande wa Jamhuri ukamilishe upelelezi na kesi hiyo
itatajwa Desemba 3 mwaka huu.
Katika kesi
hiyo, Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam,
alimuua Kanumba.
Aidha, kwa
mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu
chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji
lakini mara upelelezi wake utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania,
Kanda ya Dar es Salaam.
Post a Comment