Mshitakiwa wa kwanza Bw. Mwita Waitara Mwikwabe (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye bechi wakisubiri kuitwa mbele ya hakimu Ruth Massamu.
Vigogo wa CHADEMA washitakiwa Mwita Waitara Mwikwabe (wa pili kulia) na mshitakiwa wa pili,Dk.Kitila Mkumbo (wa kwanza kushoto mwenye miwani), wakitoka nje ya mahamaka ya hakimu mkazi Singida mjini,baada ya kesi yao kuahirishwa hadi Oktoba 8 mwaka huu.(Picha zote na Nathaniel Limu)
Kesi inayowakabili vogogo wa CHADEMA ya kumtolea lugha ya matusi mbuge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Nchema inatarajiwa kuanza kuuguruma leo asubuhi (5/11/2012) kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.
Upelelezi wa kesi hiyo,uliishakamilika na uchambuzi wa awali ulifanyika Septemba tatu mwaka huu.
Vigogo hao wanaotuhumiwa kutenda kosa hilo julai 14 mwaka huu saa kumi jioni,ni afisa sera CHADEMA makoa makuu,Mwita Waitara Mwikwabe (37) na mshauri wa CHADEMA na mhadhiri wa chuo kikuu Dar-es-salaam,Dk.Kitila Mkumbo (41).
Kesi hiyo inayovutia hisia na watu wengi,inasikilizwa na hakimu,Ruth Massamu,wa mahakama ya mkoa wa Singida.
Kwa mujiubu wa mwanasheria wa serikali,Seif Ahmed,washitakiwa bila halali,walimtusi mbunge Mwigullu kuwa ni malaya, mzinzi na mpumbavu huku akijuwa wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Seif alisema kuwa washitakiwa hao bila halali alitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali kwa lengo la viongozi wa CHADEMA kuzungumza na wananchi.