MWENYEKITI wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametumia salamu za
rambirambi Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Ndugu Amani Kabourou, kuomboleza
kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa huo, Sheikh Twakali Ali
Karago ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Novemba 9, 2012.
Katika salamu zake, Rais
Kikwete amesema: “Nimefadhaishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee
Twakali Ali Karago ambacho nimejulishwa kimetokea usiku wa kuamkia Novemba 9,
2012.” Ameongeza Rais Kikwete: “Mzee Karago alikuwa kiongozi makini na mtumishi
hodari wa wananchi. Ametuacha lakini ametuachia urithi wa kutukuka kabisa wa
utumishi wenye uadilifu na wenye kujali watu na maslahi yao. Alionyesha uongozi
imara wakati wote wa maisha yake na tutaendelea kumuenzi kwa mchango wake katika
maendeleo ya nchi yetu.”
“Nakutumia wewe Ndugu
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa, Ndugu Amani Kabourou, salamu zangu za rambirambi
kufuatia kifo cha mzee wetu huyu. Kupitia kwako nawatumia pole zangu nyingi
viongozi na wanachama wote wa CCM mkoani Kigoma kwa kuondokewa na kiongozi na
mwanachama mwenzao,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha, nakuomba kupitia kwako unifikishie salamu zangu za pole nyingi kwa wanafamilia wa Mzee Karago kwa kupotelewa na mhilimi wa familia.”
“Aidha, nakuomba kupitia kwako unifikishie salamu zangu za pole nyingi kwa wanafamilia wa Mzee Karago kwa kupotelewa na mhilimi wa familia.”
Post a Comment