Mwakilishi wa Rwanda katika
shundano la Miss East Afrika 2012
Mrembo atakae iwakilisha
Rwanda ni UMWARI NEEMA (22) ambae ana urefu wa futi 5.9 ambae ni mwanafunzi wa
mwaka wa tatu katika chuo cha Kigali Institue of Education ( KIE) na pia ni
mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo jijini
Kigali.
Mrembo
atakaeiwakilisha Nchi ya Kenya ni JOAN WAMBUI NDICHO (18) mwenye urefu wa futi
5.8 na anayetarajia kujiunga na Chuo kikuu cha Machakos University College
kusomea mambo ya utalii
Fainali za mashindano ya
Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi December mwaka huu katika
ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan,
Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na
Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu
yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani
kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza
utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na
kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East
Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es
salaam
Post a Comment