Taarifa ya Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, kwa vyombo vya habari jana ilieleza kwamba katika ziara hiyo, Dk. Slaa atafika kwenye majimbo manne ya Kigamboni, Temeke, Kinondoni na Ilala.
Dk. Slaa alianza ziara hiyo katika Jimbo la Temeke jana akitokea wilayani Karagwe, mkoani Kagera ambako alifungua na kufunga mafunzo ya darasani na vitendo ya wenyeviti na makatibu wa mikoa yote ya kichama 32 nchi nzima.
Mafunzo hayo waliyopewa wenyeviti na makatibu wa mikoa yote ya kichama nchi nzima ilikuwa ni sehemu ya kutekeleza mkakati wa na operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (MC4), yenye lengo la kuleta uongozi bora, kueneza sera sahihi, kutengeneza mikakati makini na kujenga oganaizesheni thabiti ngazi zote, kwa maendeleo endelevu ya taifa na chama.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, leo Dk. Slaa atakuwa Kigamboni, Novemba 29 ataenda Ilala na Novemba 30 atahitimisha ziara hiyo Kinondoni.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Dk. Slaa katika ziara hiyo ataataambatana na maofisa kutoka Makao Makuu ya Chadema, Ofisa wa Sera na Utafiti, Mwita Waitara Mwikwabe (Mratibu wa ziara), Subira Waziri (Naibu Katibu Mkuu Baraza la Wanawake, Bawacha), Hekima Mwasupi (Ofisa kutoka Idara ya Sheria) na Tumaini Makene (Ofisa Habari).
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment