MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, imemhukumu kwenda jela miezi mitano Katibu wa
Chadema Wilaya ya Ilemela, John Anajus huku ikiwatoza faini ya Sh620,000
viongozi wengine akiwamo Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa Chadema Taifa, Benson
Kigaila na madiwani wawili.
Hukumu
hiyo ilitolewa kufuatia watuhumiwa hao kudharau amri ya mahakama iliyotolewa na
Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani Mwanza, Angelo Rumisha kufuatia kesi namba
69/2012.
Kesi
hiyo ilifunguliwa na Henry Matata aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Kitangiri,
baada ya kuvuliwa uanachana kwa kukiuka katiba ya chama, ambaye aliweka
pinganizi la kuteua mgombea umeya Wilaya ya Ilemela.
Akitoa hukumu
hiyo, Hakimu Rumisha alisema mahakama haiwezi kudharauliwa pale inapotoa maagizo
yake, hivyo imewatia hatiani kwa kukaidi agizo lake ili iwe fundishi kwao na
wengine.
Hakimu
Rumisha aliwatoza faini ya Sh155,000 kila mmoja watuhumiwa, huku John Anajus
ambaye hakuwapo mahakamani akihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela
atakapopatikana.
Watuhumiwa
ambao walilipa faini ni Kigaila, Katibu wa Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Ilemela,
Kalod Majura, Diwani wa Kata ya Kirumba, Dan Kahungu na aliyekuwa Meya wa Mwanza
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya chama hicho, Josephat
Manyerere.
Katika
kesi hiyo, Matata anayetetewa na Wakili Salum Magongo, aliweka pingamizi
mahakamani baada ya Kamati Tendaji ya Chadema kutangaza kumvua uanachama kinyume
cha taratibu na kudai kwamba, viongozi hao kwa pamoja walishiriki kuvunja sheria
kwa kumtangaza kumfukuza udiwani.
Hivyo,
kudaiwa kupuuza amri halali ya mahakama iliyotolewa Septemba 15, mwaka
huu.
Hata hivyo, Diwani
huyo alivuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema Septemba 9, mwaka huu kutokana
na madai ya kuvunja katiba ya chama hicho, mpaka kuchaguliwa kuwa Meya wa
Manispaa ya Ilemela alikuwa amefungua kesi mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Mwanza akiomba mahakama imrejeshee uanachama wake.
Hata
hivyo, katika hatua ya kuwanusuru madiwani hao kufungwa, wananchama wa chama
hicho ambao walikuwa wamefurika mahakamani hapo walichanga Sh250,000 na
Sh370,000 zingine zililipwa na Mbunge wa Ilemela,Samson Kiwia.
Source:mwananchi
Post a Comment