Nyota wa muziki wa RNB Tanzania Diamond platnumz aelezea chanzo cha ajali
aliyopata jumamosi ya wiki iliyopita na kupelekea gari lake kukongoroka vibaya.
na hiki ndicho alichokisema nyota huyo juu ya ajali yake
"Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya
siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.
Baada ya
kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa jamaa
zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia ya
wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya
saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani nilipata ajali
ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama
mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari huwa haziko katika mwendo wa
kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele yangu na katika kujaribu
kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa
pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali
niliyokutana nayo jumamosi iliyopita.
Namshukuru sana
Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya
hapa na pale." Alisema msanii Diamond Platnumz
Hii ni pikipiki ambayo ni chanzo cha ajali..... |
Post a Comment