Kwa muda barabara ya Magomeni kwenda Sinza
kupitia Tandale eneo la Somanga, Magomeni makuti, ililazimika kufungwa kwa
magari ili kupisha umati mkubwa wa watu waliokuwa wakisindikiza mwili wa Mariam
Khamis kwenda katika mahala pake pa mwisho duniani. Mariam ambaye alikuwa
muimbaji wa
bendi ya TOT Taarab alijulikana sana kwa wimbo
wake 'Paka Mapepe' alipoteza uhai wake jana katika hospitali ya Muhimbili,
kutokana na matatizo baada ya kujifungua. Ukubwa wa umati ule ni kielelezo
kikubwa kuwa marehemu alipendwa na watu. Mungu ailaze Roho yake pema peponi
Amin
Huu ndio usafiri wetu wa
mwisho pindi tuondokako duniani ambapo dada yetu Mariam Khamis ameutumia siku ya
leo kuelekea makaburini
Mamia ya watu
walijitokeza katika mazishi ya muimbaji mahiri wa Taarab nchini Mariam Khamis
maarufu kama Paka Mapepe aliyefariki juzi wakati akijifungua. Mariam alifariki
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo mtoto wake
alisalimika.
Mazishi hayo yamefanyika
jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wasanii
wengine wa muziki wa Taarab.
Miongoni mwa wasanii
waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Mzee Yusuph
na mke wake Bi Leila, Nyota Waziri, Bi Hindu na wasanii wenzake wa kundi la
TOT.
Mwili wa marehemu
Mariam Khamis ukiwa unaelekea makaburini mapema
leo
Mamia ya watu walio
jitokeza kumsindika dada Mariam kwenye nyumba yake ya
milele
Mume wa marehemu Mariam
Khamis akiingia ndani ya kaburi tayari kwa kumzika mkewe pembeni yake ni baba
mkwe wake
Tayari kwa kupokea
mwili wa marehemu pindi uingizwapo ndani ya
kaburi
Mwili wa marehemu
Maraiam Khamis ukiingizwa ndani ya kaburi
Mazishi yakiendelea
ndani ya kaburi
Tayari dada Mariam
kashazikwa hapo zoezi la kufukia na mchanga
likiendelea
Mwanamuziki wa Taarab
Thabit Abdul naye akiiendelea na zoezi la kufukia kaburi la dada Mariam
Khamis
Na hii ndio nyumba yake
ya mwisho dada Mariam Khamis ambayo ataishi maisha yake
yote
Kaburi la marehemu dada
Mariam Khamis likiwa katika muonekano ambao tayari
lishafukiwa
Mume wa marehemu Mariam
Khamis akiwa haamini kuwa mkewe hayuko naye tena duniani kiukweli alichokuwa
akikiongea hapo pembeni ya kabuli ungekuwepo wewe rafiki yangu sidhani kama
ungeweza kuvumilia lazima ungelia pole sana kaka HAJI KIJUNGU mbele yake nyuma
yetu.
Mume wa marehemu Mariam Khamis aliporudi nyumbani tu
kutoka makaburini alimtafuta mwanaye huyo mtoto unayemuona mwenye tisheti yenye
mistari alipomuona tu akaangusha kilio cha nguvu. Mungu awatie
nguvu.
---
Mariam alikuwa muimbaji wa kundi la taarab la TOT na enzi
za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab ambayo ni
pamoja na East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5
Stars.
Marehemu Mariam Khamis ameimba nyimbo nyingi zinazofanya
vizuri katika muziki wa Taarab zikiwemo ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya Mapenzi’ na
‘Ndo basi tena’.
Mungu ailaze roho
ya marehemu mahali pepa peponi.
Post a Comment