MUUNGANO wa Vyama vya
Waandishi wa Habari nchini (UTPC) uimeikabidhi Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa
wa Arusha (APC) vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 35.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa
jana Ofisa Utawala na Fedha wa UTPC Jackosn Uiso katika ofisi za Klabu ya APC
jijini hapa na kushuhudiwa na viongozi na baadhi ya
wanachama.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi vifaa hivyo Uiso aliwahimiza viongozi kuhakikisha vinatumika kwa
wanachama ikiwa ni pamoja na kuingizia fedha Klabu.
“UTPC inawahimiza mtumie
vifaa hivi kwa uangalifu, lakini hakikisheni mnaweka utaratibu wa jinsi gani
vitawaingizia fedha za Klabu badala ya kuendelea kuvifungia,” alisema
Uiso.
Baadhi ya vifaa
vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya kudurufu, Televisheni ya Inchi 32,
Kamera kubwa ya kisasa kwa ajili ya picha za mnato, mashine ya Projector, Desk
Kompyuta na Laptop.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa APC Claud Gwandu aliwashukuru UTPC kwa kukabidhi vifaa hivyo na kuahidi
kwamba vitatumika kwa uangalifu mkubwa.
“Vifaa hivi ni vya thamani
na tunaahidi kuvitumia kwa uangalifu utakaoleta manufaa kwa Klabu na wanachama
wake,” alisema Gwandu.
Naye Katibu Mkuu wa APC
Eliya Mbonea kwa upande wake aliwashukuru UTPC kwa kufanyia kazi mawazo ya
viongozi wa Klabu nchini waliopendekeza kutumiwa vifaa vinavyolingana na
taaluma.
“Mapendekezo ya viongozi wa
Klabu yamefanyiwa kazi, awali tulikuwa tunaletewa kamera ndigo zinazowapa wakati
mgumu waandishi kupiga picha hususani viongozi wa kitaifa wanapokuja au tukio
linapokuwa mbali,” alisema Mbonea na kuongeza:
“Mfano hii Kamera ya picha
za mnato kweli hapa sasa hatuwezi kulalamika tena kwamba hatuna kamera ya kisasa
kwani Kamera hii unaweza kupiga picha ukiwa mahali popote,”
alisema.
Post a Comment