Kocha
mkuu wa timu ya Young Africans Sports Club, Mholanzi Ernie Brandts amesema
kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Coastal Union katika mchezo wa mwisho
wa kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom utakaofanyika siku ya
jumapili katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Akiongea
na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz leo
asubuhi katika mazoezi yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema
wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo anaamini
mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.
Wachezaji
wangu wapo fit wote, nadhani soka waliolicheza siku na Azam lilionekana, hizo ni
dalili tosha kuwa wachezaji wanaelewa mafunzo yangu, hivyo naamin siku ya
jumapili vijana wangu wataibuka na ushindi mzuri hali itakayotupelekea kuweza
kuendelea kushika usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara amesema
'Brandts'
Coastal
Union inayoshika nafasi ya nne katika msimo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
bara, itashuka dimbani siku hiyo ya jumapili kusaka pointi ili kujiweka katika
nafasi ya kuendelea kushika nafasi tatu za juu
Yanga
ambayo mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa mabao 2 - 0 dhidi ya timu ya
Azam FC katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki, itaingia uwanjani kusaka
pointi 3 muhimu zitakazo ifanya iendelee kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwani kama
Yanga ikishinda basi Simba na Azam hata zikishinda hazitoweza kuongoza
Ligi.
Katika
mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts ameendelea kufurahia kuwepo kwa
wachezaji wake wote, kitu kitakachopelea kumtumia mchezaji yoyote atakayetaka
kumtumia kwa mchezo huo wa jumapili, kwani hakuna mchezaji aliye majeruhi
.
Vijana
wa jangwani kwa sasa wanakamata nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara kwa kufikisha point 26, mbele ya Azam yenye pointi 24 na
Simba yenye pointi 23 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo
12.
Post a Comment