Inawezekana kweli kabisa kuwa mapenzi
yanapoanzia ndipo ugumu unapoishia, na aliyesema Love is a cure huenda kwa hii
story akawa right.
Mchumba wa the West Coast rapper Game, Tiffney
Cambridge hivi karibuni ameelezea uhusiano wake na mkali huyo wa michano
na kwamba walikutana muda mfupi baada ya Game kutoka G-Unit katikati ya miaka ya 2000.
Mrembo huyo ameelezea mahusiano yao
yalivyoanza na kushamiri na kwamba walikutana wakiwa katika wakati mgumu sana na
walisaidiana kusolve matatizo yao kwa kutumia mapenzi tu. Walivyokutana
sasaa..., ni story nzuri hasa ukimjengea picha Game aliyolainika kwenye mikono
ya mrembo huyu.
“kupitia mtoto wa dada angu, dada yake
Game alikua anatengeneza nywele kwenye barbershop yake, kwa hiyo nilikuwa naenda
kutengeneza nywele pale, kwa hiyo nilikuwa namuona Jayceon pale,” alisema
Cambridge alimtaja Game kwa jina lake la kuzaliwa.
Mrembo huyo alielezea kuwa Game alikuwa
kama anamuwindawinda kwa kwa maneno flani ya uchokozi hata walipokuwa wanakutana
nje ya maeneo ya barbershop hiyo, “can I take you out? and all that kind of
stuff”.
Cambridge aliendelea kufunguka,
“...tulikuwa na shangwe kibao tukiwa pamoja. Wakati mama yangu alipofariki
alinisaidia sana kunituliza, na mimi nilimsaidia alipokuwa anatoka kwa mara ya
kwanza G-Unit. Kiukweli tulidevelop urafiki wa kipekee japokuwa ilikuwa ndio
kama kufall in love hivyo.” Wakati Game anatoka G-Unit alikuwa na challenge sana
na media zilimuandama na mengi ya kumuumiza yalitoka kwa 50 Cent aliyemuona kama
a rebel.
Game na Cambridge sasa ni wachumba na
kwa mujibu wake Game Alishapropose kwake mara nyingi na wakati mwingine akiwa
amekasirika kabisa lakini Game alipenyeza maneno mazuri ya kimapenzi akitaka awe
mkewe wa halali, na hii ilisababisha wakati mwingine amkatalie kwa sababu
alikuwa amekasirika.
hivi karibuni Game alielezea kuwa
amejaribu sana kumuweka mbali mchumba wake huyo na media kwa sababu hataki
kumuumiza, "nilimuweka mbali kwa sababu nilifeel ingeweza kumuumiza au kumdhuru"
alisema Game. "Na sikuwa tayari naye hakuwa tayari, ni mengi ya kudeal nayo na
kwa upande mwingine, I was trying to keep it player.”
Post a Comment