Warembo wanaoshiriki mashindano ya
Miss East Africa 2012 wanatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es salaam
wakitokea katika Nchi mbalimbali tayari kwa mashindano hayo makubwa yatakayo
fanyika tarehe 07 07 December katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
wakati huo huo Mtangazaji mashuhuri wa Mnet na ambae amewahi kuwa mshindi wa Big
Brother Africa, Gaetano Kagwa anayeishi Afrika Kusini ndiye atakaekuwa MC wa
mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika jijini dar es
salaam
Fainali za mashindano ya Miss East
Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi,
Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius na warembo mbalimbali wa
Afrika mashariki walioshindana katika Nchi mbalimbali za
Ulaya
Mashindano ya Mwaka huu
yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani
kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza
utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na
kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa
yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es
salaam
Post a Comment