Muimbaji mahiri wa kike hapa nchini
Judith Wambura (kulia) almaarufu kwa jina la Lady Jay Dee akizungumza na
waandishi wa habari leo katika mgahawa wake wa ‘Nyumbani Lounge’ uliopo jijini
Dar es Salaam na kutambulisha rasmi kipindi chake kipya cha luninga
kitakachoitwa‘Diary ya Lady Jay Dee’.
Amesema madhumuni ya kipindi hicho ni kuleta burudani
tofauti kwa wapenzi wa muziki wake na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla,
vilevile kitatoa fundisho na changamoto kwa wasanii chipukizi kujua wasanii
wakongwe wamepitia katika vikwazo gani.Lady Jay Dee amesema
kipindi hicho kitaonyeshwa ndani ya East Africa Television kuanzia tarehe 18
Novemba mwaka huu kila siku ya Jumapili.
Aidha ametumia fursa hiyo kutoa
wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kushiriki katika kudhamini vipindi
vinavyobuniwa kama hivyo ili kuweza kutoa ajira kwa wasanii na wadau wengine wa
sekta ya muziki na burudani.Kushoto ni Mkuu wa Vipindi wa East Africa TV Bi.
Lydia Igarabuza
Mkuu wa Vipindi wa East Africa TV
Bi. Lydia Igarabuza akizungumzia jinsi stesheni hiyo ilivyopokea kwa shangwe
kipindi hicho na kuwa kitakuwa hewani Jumapili saa 3 usiku kuanzia Novemba 18 na
kuwataka vijana wa Afrika Mashariki kukitazama ili kujifunza mengi kutoka kwa
watu ambao tayari wanamafanikio kupitia tasnia ya muziki.
Post a Comment