Klabu ya soka ya
Manchester United imepunguza deni lake katika robo ya kwanza ya mwaka huu, baada
ya familia ya Glazer inayomiliki timu hiyo, kulipa milioni
62.6.
Kwa jumla, deni
lilipungua na kusalia pauni milioni 359.7, katika kipindi cha miezi mitatu kabla
ya tarehe 30 mwezi Septemba, mwaka 2012.
Deni hilo limepungua kwa
asilimia 17, ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.
Mapata ya Manchester
United yalipanda kwa asilimia 3.4, na kufikia faida ya pauni milioni 76.3, klabu
hiyo ya Old Trafford imeelezea.
Lakini faida kutokana na
utangazaji wa mechi zake ilipungua kwa asilimia 37.4, na kufikia pauni milioni
13.7, hasa kutokana na kubadilishwa kwa ratiba za mechi.
Klabu kilicheza mechi
moja ya klabu bingwa, ilhali msimu uliopita ilicheza mechi mbili, na vile vile
ilipungukiwa kwa mechi mbili zilizotangazwa moja kwa moja, ikilinganishwa na
msimu wa awali.
Tofauti hizo
zilisababisha hasara ya pauni milioni 5.6, ilhali klabu kina matumaini kitakuwa
katika hali bora zaidi kwa kucheza mechi zaidi za klabu bingwa.
Manchester United
ilipungukiwa kwa milioni 2.6, kwa kucheza mechi chache za klabu bingwa, hasa kwa
kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Premier, msimu 2011-12,
ilikilinganishwa na msimu 2010-11.
Klabu, kwa sasa
kinaongoza katika ligi kuu ya Premier.
Post a Comment