|
Kijana Priva Elian wa Rombo mkoani Kilimanjaro,
amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni
kugombaniwa na wanawake wawili.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo,
walidai kijana huyo alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.
Walidai kuwa alifikia uamuzi , mwaka huu saa 1:30
asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa
akiupata kutoka kwa wanawake hao.
Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua
uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa
achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.
“Hatujui
alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya
kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani
ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo
la kusikitisha. |
on Friday, November 16, 2012
Post a Comment