Maafisa afya nchini
Uganda wamesema kwamba watu watatu wamekufa baada ya kuugua ugonjwa wa Ebola,
lakini serikali haina uhakika kuhusu kilichosababisha visa hivi vilivyotokea
Luweero.
Inashukiwa kuwa watu
wengine watano wameambukizwa,wawili kati yao wametengwa katika wodi maalum
katika hospitali kuu ya Mulago, mjini Kampala.
Hii ni mara ya tano kwa
kuzuka kwa Ebola nchini humu katika miaka 12 iliyopita.
Mlipuko wa ugonjwa huo
mnamo Julai mwaka huu ulisababisha vifo vya watu 17.
Inakadiriwa kuwa watu 17
waliaga dunia magharibi mwa Uganda, kutokana na ugonjwa huo mwezi Julai mwaka
huu.
Kwa mujibu wa shirika la
madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres (MSF), hakuna maafa yoyote
yaliyoripotiwa kuhusiana na ugonjwa huo hatari tangu mwezi
Agosti.
Waziri huyo wa Afya
ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha
kuwa watu hao waliaga dunia kutokana na ugonjwa huo wa Ebola katika eneo la
Luwero, takriban kilomita sitini kutoka mki mkuu Kampala.
Lakini amesema mwanaume
mmoja kutoka eneo hilo, pia aliaga dunia mwezi uliopita, kutokana na kile
kilionekana kuwa dalili za ugonjwa huo, lakini hakuna uchunguzi uliofanyika
kuhusiana na kifo hicho.
Watu watano ambao ni
jamaa wa karibu wa walioaga dunia, wanaendelea kuchunguzwa na madaktari. Wawili
kati yao wamelazwa katika chumba maalum katika hospital kuu ya kitaifa ya Mulago
mjini Kampala.
Hakuna tiba maalum
inayojulikana ambayo inaweza kutumika kutibu ugonjwa huo, lakini wagonjwa hupewa
dawa za kawaida za kinga pamoja na zile za kupunguza maumivu na kutibu Malaria
ili kuongeza kinga mwilini.
Asilimia Tisini ya watu
wanaogunduliwa kuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo wa Ebola huaga dunia,
na katika kipindi cha miaka Kumi na mbili iliyopita kumekuwa na visa kadhaa vya
mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.
Takriban asilimia 50 ya
yatu 425 ambao walikuwa wameambukizwa virusi hivyo waliaga dunia mwaka wa
2000.
Wizara ya Afya, pamoja
na Shirika la Afya Duniani walikuwa wametangaza kwamba ugonjwa huo ulikuwa haupo
tena Uganda. Lakini umezuka tena.
Wanaougua Ebola hupata
homa kali, huvuja damu, na viungo vyao vya mwili vya ndani huacha kufanya
kazi.
Waganda wengi
wanashangaa ni kwa nini nchi yao hukumbwa mara kwa mara, lakini serikali inasema
kwamba ni kwa sababu mifumo yao ya uchunguzi imeboreka zaidi.
Hali kadhalika, katika
mwezi mmoja uliopita watu tisa wamefariki baada ya kuugua ugonjwa wa homa
unaoambukiza wa Marburg, unaofanana na Ebola.
Post a Comment