· Wateja
kupata taarifa kupitia SMS, Facebook na
Twitter.
· Yatoa
pongezi kwa vyombo vya habari na timu.
Dar
es Salaam Mdhamini
Mkuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania, imewekeza katika kuwawezesha mashabiki wa soka kupata taarifa na
matukio ya mechi zote za ligi hiyo kupitia njia ya simu za kiganjani na
intanet.
Kupitia mifumo
mbalimbali ya kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata matokeo ya mechi
mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na ujumbe mfupi wa maneno na
mitandao ya kijamii.
Akizungumzia hatua hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema, Mtandao wa Vodacom
una miundombinu ya kutosha na unaongoza katika masuala ya teknolojia. Hivyo
itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa soka walioko ndani na nje ya nchi
kujua matukio mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom.
“Licha ya ligi yetu
kuonekana katika kituo cha Televisheni cha Super Sport. Tumejipanga sasa
kuhakikisha inakuwa katika mitandao mbalimbali muda wote kwa kila mchezo na kila
tukio katika soka, Mashabiki watapata taarifa za ligi popote watakapokuwa,”
alisema Meza na Kuongeza kuwa, “Kupitia intanet matukio haya yatapatikana
kupitia Facebook na Twitter na mitandao mingine ya
kijamii.”
“Ili kupata matokeo na
taarifa mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa Vodacom atatakiwa kupiga*149*01# kisha
atachagua VODACOM
FLAVA na akisha kujiunga na huduma hiyo itakayo muwezesha kupata taarifa
na matokeo ya mechi mbalimbali”
Aliongeza kuwa, “ Kwa
wateja wanaotumia facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi kwani huduma hizo
zinatolewa bure na Vodacom, hivyo mashabiki wa soka watatembelea Ukurasa wetu wa
facebook na Twitter na kupata taarifa mbalimbali kuhusu ligi na wengine
kujishindia zawadi kwa kujibu maswali mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za
ligi,”
Aidha Mkurugenzi huyo
alitoa Pongezi kwa Vyombo vya habari kwa kazi kubwa inayofanya katika
kuwahabarisha watanzania kuhusu michezo mbalimbali hususani ligi kuu ya Vodacom
kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na Mitandao ya
kijamii.
“Vyombo vya habari ni
wadau wakubwa na wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa taarifa hizi wanastahili
pongezi, nasi tunaangalia namna ya kuwaunga mkono kwa namna moja ama nyingine
katika jitihada za kukuza soka la Tanzania na tunaamini tutafika
mbali.”
Mkurugenzi huyo
alihitimisha kwa kutoa pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligi kwa
kusema kuwa zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa ni ishara ya ukuaji wa
soka katika soka la Tanzania ambalo ndio lengo kuu la
Vodacom.
“Ligi sasa imekuwa na
msisimko kila timu inajitahidi kushinda kila mech,hadi sasa timu zote zimeonesha
kiwango kikubwa na soka la kuvutia tunatarajia maendeleo haya yataleta tija hata
kwa timu yetu ya Taifa kufanya vizuri. Vipaji vingi vinaonekana na ajira kwa
vijana imeongezeka kupitia michezo,” alihitimisha
Meza.
Kampuni ya Vodacom
katika kuongeza msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa ofa mbalimbali msimu huu
kwa kuwawezesha wateja wake kupata SMS 50, Muda wa maongezi wa dakika 30 na MB
50 kwa shilingi 400 Ili kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki. Pamoja na mambo
mengine kampuni hiyo inaangalia namna ya kutoa adha ya ukataji tiketi kwa wateja
wake kutumia huduma ya M - pesa kununua tiketi za mechi
mbalimbali.
Mwisho
Post a Comment