Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Abdallah Lutavi
akiwasha taa kuzindua mradi wa umeme wa nishati ya jua kwenye shule ya Sekondari
Selous iliyopo Wilaya ya Namtumbo uliyofadhilwa na kampunin ya Mantra Tanzania
kwa shilingi milioni 28.7. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra
Tanzania Asa Mwaipopo na mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa(wapili kushoto). (Na
Mpiga Picha Wetu).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra
Tanzania Asa Mwaipopo (kulia) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi
mradi wa umeme wa nishati ya jua kwenye shule ya Sekondari Selous iliyopo Wilaya
ya Namtumbo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Abdallah Lutavi.
Mbunge wa Namtumbo Vita
Kawawa(kushoto) akibadilisha mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Abdallah
Lutavi(katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi mradi wa umeme wa nishati ya jua
kwenye shule ya Sekondari Selous iliyopo Wilaya ya Namtumbo.Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mantra Tanzania Asa Mwaipopo.
Na Mwandishi
Wetu, Namtumbo.
KAMPUNI
ya Mantra Tanzania Limited imeikabidhi mradi wa umeme wa nishati ya jua wenye
thamani ya shilingi milioni 28.7 kwa shule ya Sekondari ya Selous iliyopo Wilaya
ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma, utakaosaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule
hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla
ya kukabidhi mradi huo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania Asa Mwaipopo
alisema kuwa kampuni yake imejikita katika kusaidia miradi mbalimbali katika
mkoa huo.
Mwaipopo alisema kuwa mradi
utawasaidia wanafunzi wa shule hiyo kujisomea wakati wa usiku pamoja na kusaidia
kufukuza wanyama wakali waliyopo eneo la shule hiyo.
“Baada
ya kumalizika kwa mradi huu,tunaimani kuwa wanafunzi watapata fursa nzuri ya
kujisomea katika mazingira tulivu. Tunamatarajio kuwa mradi huu utasaidia kuinua
kiwango cha elimu cha shule hii na nimatarajio yetu kuwa utatunzwa vizuri kwa
matumizi ya kizazi kijacho,” alisema Mwaipopo.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Abdallah Lutavi aliyekuwa mgeni rasmi
katika hafla hiyo alikuwa na mategemeo makubwa kuwa mradi huo na kusisitiza kuwa
mradi huo utakuwa nguzo ya kuboresha elimu katika shule hiyo.
Lutavi
alisema kuwa mradi huo utausaidia mpango madhubuti wa wilaya wa hiyo unaolenga
kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba 2013 kila shule katika wilaya hiyo inakuwa na
maabara.
“Mpaka
sasa, ni shule sita tu ndiyo zenye maabara. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa shule
zote katika wilaya zinakuwa na maabara. Maabara hizo haziwezi kukamilika bila
umeme.
“Tunatoa shukrani zetu kwa
Mantra Tanzania kwa mchango wao na tutahakikisha kuwa mradi unatunzwa vizuri,”
alisema.
Aidha,
Mbunge wa Namtumbo, Mh. Vita Kawawa wakati wa tukio hilo alitoa wito kwa uongozi
wa wilaya kuhakikisha kuwa ujenzi wa mabweni ya wavulana unapewa kipaumbele
wakati wa bajeti ya fedha ya wilaya ijayo.
“Wavulana wanalazimika
kutembea mpaka kilometa tano hali ambayo inaweka maisha yao hatarini dhidi ya
wanyama wakali. Ombi langu ni kuwa ujenzi wa mabweni ya wavulana upewe
kipaumbele kikubwa katika bajeti inayofuata,” alisema.
Awali
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule, Bw. Henry Milanzi alibainisha kuwa shule yake
inakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama pamoja na
kutokuwepo na ukuta katika eneo la shule.
Post a Comment