WASHANGAE
kwanza kidogo kwenye hiyo picha halafu nikwambie kitu. Hawa mapacha Chidimma na
Chidiebere Aneke wanatamani kuolewa na Peter & Paul Okoye wanaounda kundi la
muziki la P Square.
P-Square ni mapacha kama ilivyo kwa hao
mabinti. Lakini wao watamani kuolewa na wavulana ndugu. Wakizungumza na gazeti
moja la Lagos, Nigeria wametamka kwamba hao jamaa wakipeleka posa watawasikiliza
na kufikiria mara mbili.
"Kama wakitufuata hatuwezi kukubali moja kwa
moja bila kumtanguliza Mungu. Kwa Ukristo tulionao hatudhani ni kwamba
nikumkubalia kila mtu anayetaka ndoa," alisema Chidimma.
"Ni watu wazuri lakini hatuwezi kusema ndio moja kwa moja, hii ni kwa sababu tukishaolewa tumeolewa. Hatuwezi kutoka tena, ndiyo maana tunapaswa kuwa makini kwenye uamuzi. Fedha si kila kitu, Mungu ndiye anapaswa kukuonyesha kwamba huyu ni mkeo au mumeo.
Post a Comment