Loading...
Rais 'akabidhi zigo' wakuu wa mikoa kujenga maabara
RAIS wa Jakaya Kikwete, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini, kujenga maabara kwa kila shule ya sekondari katika kipindi cha miaka miwili kuanzia sasa.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo juzi wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi mkoani Singida, waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mji mdogo wa Itigi.
Alisema maabara ya sayansi ni muhimu katika maendeleo ya wanafunzi kujifunza kwa nadharia na vitendo.Kikwete alisema kutokana na umuhimu huo, kunahitajika ushirikiano kama ule ulioonyeshwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari za kata.
“Kuhusu uhaba wa walimu, Serikali imejipanga vizuri na inaendelea kupunguza uhaba huu na lengo ni kuumaliza mapema iwezekanavyo,” alisema.
Rais Kikwete ambaye alikuwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani hapa ambapo alizindua, kufungua miradi ya barabara na maji, pia aliagiza barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa zikiwamo za lami, zilindwe na kutunzwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Alisema Serikali kwa upande wake, inaendeleza mikakati yake ya kujenga barabara za kiwango cha lami kwa lengo la kuunganisha mikoa yote iweze kufikika kwa urahisi.
“Leo nimezindua ujenzi wa barabara hii ya kutoka Manyoni-Itigi-Chaya mpakani na Tabora. Ujenzi huu hauwezi kuishia hapo, tutaendeleza hadi mkoani Kigoma mjini,” alisema.
Awali, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema ujenzi wa barabara hiyo ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa kilometa 89.3 unatekelezwa na Kampuni ya China ya Sinohyadro Corporation Limited kwa gharama ya Sh109.6 bilioni.
“Mheshimiwa kampuni hii ya Sinohyadro, inaendelea kufanya vizuri katika kujenga barabara hii. Utendaji wao unaleta matumaini kuwa kazi waliyopewa, itakamilika kwa wakati,” alisema.
BLOG RAFIKI
-
-
-
Kwa Undani5 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment