Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANESCO BADO HALI SI SHWARI


Msemaji wa Tanesco Badra Masoud

BAADA ya kuhamishwa kwa zaidi ya wafanyakazi 150 wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kutokana na sababu mbalimbali, imefahamika kuwa hatua inayofuata ni kuwahamisha wahandisi wake wa vitengo mbalimbali.
Mwananchi lilibaini kuhamishwa kwa mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo hatua iliyoelezwa kuwa ni ya kuvunja mtandao wa wizi na hujuma.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa ni mabadiliko ya kawaida.
Akizungumza na gazeti hili jana Dar es Salaam, Msemaji wa Shirika hilo Badra Masoud alikana taarifa za kwamba mabadiliko hayo yalitokana na ubadhirifu na hujuma na kwamba ni mabadiliko ya kawaida kama ofisi zingine.
“Hakuna ubadhirifu wowote katika mabadiliko hayo bali ni hali ya kawaida kama ofisi zingine zinavyofanya uhamisho wa wafanyakazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine,”alisema Masoud.
Wakati akisema hayo, habari zaidi ambazo Mwananchi imezipata, zinasema kuwa baada ya kuhamishwa wasimamizi na watu wengine wa kawaida, hatua inayofuata ni kuwahamisha baadhi ya wahandisi.
“Mpango unaofuata ni kuhamisha vituo vya kazi wahandisi kutoka maeneo mbalimbali…Wale wa kwanza walikuwa wasimamizi na watu wa kada nyingine za utawala,” kilipasha chanzo hicho.
Badra alisema kila mfanyakazi anahamishwa na kupelekwa katika idara ambayo ana uwezo nayo na mchakato huo utaendelea katika idara zingine.
Mwananchi lilitaka kujua kama kuna mabadiliko yatakayofanyika kwa upande wa wahandisi wa shirika hilo, alisema utaratibu huo utafanyika kama ule wa awali kulingana na uwezo wa wafanyakazi hao.
“Kwani nani kawaambia uhamisho huo umetokana na ubadhirifu kwani ofisi zingine wanapofanya mabadiliko ya uhamisho mbona hakuna mtu anayeshangaa iweje sisi tufanye mabadiliko muanze kuhoji?,” alihoji Masoud.
Masoud alikana taarifa za ubadhirifu badala yake alisisitiza kwamba watu wasidhani kuna hujuma bali shirika limeamua kufanya mabadiliko ya kawaida.
Hata hivyo habari ambazo Mwananchi ilizipata awali na kuthibitishwa na uongozi wa juu wa Tanesco, zilieleza kwamba hadi sasa wafanyakazi 190 wameishakabidhiwa barua za kuhamishwa na nusu ya watumishi hao ni wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo wafanyakazi 95 wamepanguliwa kutoka katika mikoa ya Tanesco iliyopo katika Jiji la Dar es Salaam pekee na wamehamishiwa mikoani wanatakiwa wawe wameripoti katika vituo vyao vya kazi ifikapo Novemba 15, mwaka huu.

Habari kutoka ndani ya Tanesco zilieleza kuwa sababu za kupanguliwa kwa wafanyakazi hao, wengi wakiwa ni wasimamizi wa ndani na nje (Supervisors na foremen), ni kuvunja mtandao wa wizi na hujuma hasa katika Jiji la Dar es Salaam.
Taarifa hizo zilieleza kuwa huenda Tanesco ikiwa imepata hasara kubwa ya fedha kutokana na wizi wa umeme ambao umekuwa ukifanywa na maofisa wa Shirika hilo kwa kusaidia wateja kuchezea mita na kupata umeme bure.


CHANZO: MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top