Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI ) wamesema kuwa wateja wao waliokamatwa siku 17 zilizopita kwa tuhuma za kuchochea vurugu kisiwani Unguja, hawatendewi haki na wanapata mateso makubwa gerezani wanakoshikiliwa ikiwemo kunyolewa ndevu.
Mawakili hao wakiongozwa na Salim Tawfiq wanasema kwa sasa wateja wao hawapaswi kutendewa visa kama hivyo kwa kuwa bado ni watuhumiwa na kwamba hawajatiwa hatiani.