Meneja wa Baraza la Habari
kanda ya Zanzibar(MCT)Suleiman Seif Omar akifafanua jambo kwa Waandishi wa
Habari hawapo pichani kuhusu tamko la Tume ya utangazaji Zanzibar kupiga
marufuku kuripoti taarifa za UAMSHO zenye kuashiria uvunjifu amani kushoto ni
Kaimu Katibu Mtendaji wa MCT John P.Mireny
………………………….
Na Maelezo
Zanzibar
Vyombo vya habari nchini vimeshauriwa
kujiepusha kuandika habari za uchochezi zinazoweza kuhamasisha chuki ndani ya
jamaii na hatimaye kuvuruga amani na utangamano wa
nchi.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Katibu
Mkuu wa Baraza la Habari Tanaznia (MCT) John Mireny alipokuwa akizungumza na
Waandishi wa Habari katika Ofisi za Baraza hilo Mlandege Zanzibar kuhusiana na
Tamko lililotolewa na Tume ya Utangazaji Zanzibar la kupiga marufuku matangazo
yote yanayohusiana na vurugu zinazohusishwa na wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO
Zanzibar.
Amesema pamoja na ukweli kwamba Baraza
la Habari linatambua na kutetea kwa nguvu zote uwepo wa uhuru wa Vyombo vya
habari na uhuru wa kujieleza, Baraza linasisitiza kwamba vyombo hivyo vinawajibu
mkubwa wa kulinda amani na jamii kwa ujumla.
Amesema Tume haikukosea kupiga marufuku
taarifa za Jumuiya ya UAMSHO zinazoashiria fujo na uvunjifu wa amani na kwamba
hizo ni taarifa ambazo hazikubaliki kutolewa katika vyombo vya
habari.
Hata hivyo ameongeza kuwa taarifa
zinazohusu UAMSHO ambazo hazihusiani na fujo na uvunjifu wa Amani zinaweza
kutolewa na vyombo vya habari nchini ili kuipasha jamii habari za Jumuiya
hiyo.
Ametoa mfano wa habari za Jumuiya ya
UAMSHO ambazo zinaweza kuripotiwa kuwa ni pamoja na mwendelezo wa Kesi inayohusu
Viongozi waandamizi wa Jumuiya hiyo Uchimbaji wa Visima habari za kimaendeleo
uchumi na kadhalika .
Nae Meneja wa Baraza hilo Kanda ya
Zanzibar Suleiman Seif Omar aliwataka wandishi wa habari kuwa wadadisi na
wafatiliaji kwa baadhi ya taarifa zinazo tolewa na vyombo vya dola na isishie
kukaa kimya bila yakupata ufafanuzi .
Aidha alifahamisha kua iwapo
mwandishi hakua makini katika kuandika habari zake na kuandika habari za
utenganishaji jamii, atambue kua jamii hiyo itakua ni vigumu kuirejesha katika
maelewano jambo ambalo halifai kwa mwandishi kufanya
hivyo.
“Neno moja linaweza kuleta maafa kwa
jamii kwa hivyo wandishi wanapaswa wawe makini katika kutekeleza kazi zao kwani
amani ikitoweka ni vigumu kuirejesha”alisema Suleimani Seif
.
Aliwakumbusha waandishi kua fani ya
uandishi wa habari inamaadili yake yanayopaswa kufuatwa katika kuandika habari
na iwapo hayakufuatwa na kutanguliza ushabiki ni hatari na inaweza kusababisha
mtafaruku ndani ya jamii.
Post a Comment