Mshambuliaji
wa Barcelona Lionel Messi ameamua kufunguka na kuweka sawa kwamba hana
matatizo yoyote na David Villa.
Wawili hao walitoleana maneno makali wakati
wa mechi uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Barcelona na Granada mapema msimu
huu, na vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba wawili hao wamekuwa na
mahusiano mabovu tangu kutokea kwa tukio hilo.
Jaokuwa Messi amekuja
kuweka wazi kwamba tofauti zao ziliishia pale pale uwanjani.
"Ishu ile
ilileta mtafuruku kiasi baada ya tukio lile kutokea. Lakini kwa hakika ugomvi
ule uliishia pale uwanjani," Messi alikaririwa akisema kupitia gazeti la El
Mundo Deportivo. "Sasa hatuna tofauti zozote tunapatana kama zamanina kama
ilivyo kwa watu wengine kwenye chumba cha kubadilishia nguo."
Aliongeza,
"David ni mtu mzuri ambaye hagombani na mtu yoyote. Ni vigumu sana kugombana na
mtu mwenye tbia kama zake.
"Tuliongea kuhusu kilichotokea, na kwa hakika
hatuna tofauti zozote kwa sasa." - Alimaliza Messi.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Duniani Leo52 minutes ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment