MUIGIZAJI wa
siku nyingi Jennifer Mwaipaja
‘Shumileta’, amedai kuwa maisha
yake ni ya kawaida na haishi kwa kujiumiza kichwa kwani kile anachokipata
kinamtosha na hajawahi kutumia njia za mkato kupata mali kama wengine
wanavyofanya, kwa kujiuza kwenye hoteli kubwa kubwa ili tu wapate wanaume
wenye pesa nyingi.
Wakati alipozungumzia juu ya wasanii wanaojiunza
kwenye hoteli kubwa kubwa, mwandishi wa mtandao wa DarTalk alitaka kujua kiundani ishu hiyo, ndipo alipodai kuwa
wapo baadhi ya nyota wanaofanya kazi hiyo kwa kuwa hawaithamini miili yao na
ndiyo maana wanafanya hivyo.
Akiongea na DarTalk, Shumileta alidai kuwa uwepo wake kwenye game kwa muda mrefu
kumemfanya ajifunze mambo mengi na huwa anashika kichwa pale anapowaona wasanii
waliokuja juzi kwenye tasnia hiyo wakijiona kama wakongwe wakati hakuna kitu
wanachokijua.
Alisema
kuwa yapo mabaya mengi anayoyajua lakini wasanii wengine anapowaelekeza wamekuwa
wajuaji sana hivyo anawaacha na anawachukulia kama wao wanavyotaka, lakini wengi
wanapotea kutokana na kutojua wanatakiwa waishi vipi ili kwenda sawa na umaarufu
walionao.
“Ukubwa
dawa unajua kuna wasanii wamekuja jana lakini wanashindwa kuelewa kwamba yule
uliyemkuta lazima umpe heshima yake wao hawajui hilo, kwa sababu tu
wanafanya vizuri majina yanajulikana basi, lakini kuna mambo ambayo wanafanya
wanapotea na watu kama sisi tunayajua lakini tunashindwa kuwaambia kwa sababu
wanakauli za kuudhi,” alisema.
Post a Comment