.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(Tazara), akizungumza katika mkutano wa wafanyakazi hao uliokuwa na lengo la
kushinikiza kulipwa mishahara yao ya Septemba na Oktoba, mwaka huu. Mkutano huo
uliitishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu) jijini Dar es Salaam jana.
**************Wakizungumza katika ofisi za TAZARA jijini Dar es Salaam kwa sharti la kutotajwa majina yao katika vyombo vya habari kwa kuhofia kuhatarisha ajira zao, wafanyazi hao waliokuwa wamejikusanya katika vikundi vidogo vidogo wamesema kuwa ni mwezi wa pili sasa hawajalipwa mishahara yao.
Wamesema wamekuwa wakiomba malipo hayo kwa muda mrefu bila mafanikio hali iliyosababisha waamue kusitisha huduma mpaka hapo watakapopatiwa ufumbuzi wa kupewa malipo yao.
Wamesema kutolipwa mishahara hiyo ya miezi miwili kumewafanya waishi katika mazingira magumu na familia zao kwani wao ndiyo wanaotegemewa na kuwa kila wanapodai fedha hizo madai yao yamekuwa yakipuuzwa na viongozi kukataa kukutana nao hali iliyosababisha waingie katika mgogoro huo wa kimaslahi na TAZARA.


Post a Comment