jiji
la Mwanza.
Mtu
huyo ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake
ametambuliwa
kwa jina moja tu la Greda.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa leo mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari wa
halmashauri ya jiji la Mwanza wakiwa katika maeneo yao ya
kazi
eneo la barabara ya Pamba kwenye stendi ya zamani ya mabasi ya Tanganyika karibu
na soko kuu la jiji hilo, wakiwa katika operesheni zao za kawaida za kusafisha
jiji walikamata bidhaa zilizokuwa zimepangwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi
kisheria wakiwa kwenye eneo hilo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga
alimrukia mgambo wa jiji shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya sime kwa
nia ya kumdhuru.
|
Maganda
ya risasi zilizo tumika. |
Baada
ya tukio hilo wamachinga waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao
wa jiji mawe ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi
hewani kuwatawanya wamachinga hao waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa
seleka hilo, kwa bahati mbaya moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga debe
mmoja upande wa kushoto na kufariki papo hapo.
Machinga
mwingine amejeruhiwa kwenye mkono wa kushoto katika kiwiko, naye dereva wa
magari ya biashara za kusafirisha mizigo wa gari aina ya Kenta, magari ambayo
hupaki katika eneo hilo amejeruhiwa upande wa kushoto kichwani na kukimbizwa
hospitali ya rufaa Bugando kwa matibabu.
|
Mmoja
wa viongozi wa akiwatuliza wamachinga wenzake kupata kumsikiliza mkuu wa polisi
(OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu.
. |
|
Mkuu
wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. akizungumza na
wafanyabiashara hao wadogo (wamachinga) kuendelea na kazi kwa kufuata sheria
wakati jeshi hilo likifanya uchunguzi wa tukio
hilo. |
|
Maduka
mengi hususani yaliyo karibu na eneo la tukio yamefungwa kufuatia seleka
hilo. |
|
Makutano
ya barabara za Liberty na Nyerere ambalo muda wote huwa na pilikapilika za
kibiashara likionekana tupu kutokana na vurugu hizo zilizo sababisha
wafanyabiashara kukimbia na kufunga biashara zao kuhofia vurugu
hizo. |
|
Mmoja
kati ya viongozi wa wamachinga akizungumza na wenzake kuwasihi kulinda utulivu
ili haki yao isipotee. |
Post a Comment