Mke wa
balozi wa Ireland nchini Tanzania (wa kwanza kushoto), Sarah Colins akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika ubalozi wa Uswisi,
kuhusu maonesho ya hisani yatakayonyika siku ya jumamosi jijini Dar es Salaam
yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi katika mazingira
magumu .na kufunguliwa na mke wa Makamu wa Rais Bi. Asha Bilal siku ya jumamosi.
Pamoja nae ni Mwenyekiti wa kundi hilo Juliana Parroni (Switzeland) na Keiko
Okada (Japan).
Mwenyekiti
wa kundi la wake wa mabalozi nchini (DSG) Juliana Parroni,(kulia) akizungumza na
waandishi wa habari, juu ya maonyesho ya hisani yatakayo fanyika siku ya
jumamosi na kufunguliwa na Mke wa makamu wa Rais, Bi Asha Bilal kwa ajili ya
kuchangisha fedha kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu. Kutoka kushoto ni
mke wa Balozi wa Namibia Aletha Aisaack, Sara Colins (Ireland) Keiko Okada
(JAPAN) na Kaisa Alapartanen (Finland).
Mke wa
Balozi wa Japani nchini Tanzania (wa kwanza kutoka kulia) Keiko Okada,
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari juu ya Maonyesho ya hisani
yatakayofanyika mwisho wa wiki ili kuchangisha fedha kwa ajili ya makundi ya
watu wasiojiweza, pamoja nae kutoka kushoto ni Mke wa Balozi waIreland Sarah
Colins na katikati ni Mwenyekiti wa umoja huo Bi. Juliana Paroni. Maonyesho hayo
yatafunguliwa na Bi. Asha Bilal Mke wa makamu wa
Rais.
========
======= =======
Maonyesho ya Hisani
2012
Siku ya
furaha kwa mafanikio ya Watanzania.
Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Asha Bilal, anatarajia
kuwa Mgeni rasmi katika Maonyesho ya Hisani yaliyoandaliwa na kundi la wake
wa Mabalozi nchini. (DSG)
Maonyesho
hayo yatakayo fanyika Novemba 17, mwaka huu katika viwanja vya Shule ya
Kimataifa ya Tanganyika, jijini Dar es Salaam, hufanyika kila Mwaka kwa ajili
ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye mahitaji maalumu hasa
wanawake, watoto na walemavu wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni mala ya
pili Mke wa Makamu wa Rais kuendesha uchangishaji huo.
Mwaka
2011, Umoja huo kupitia maonyesho ya hisani ulikusanya jumla ya Shilingi milioni
73, ambazo zilisambazwa kama ufadhili kwenye miradi 15 ya hisani na taasisi
binafsi Tanzania Bara na Visiwani, michango hiyo hufikia shilingi milioni 15 kwa
kila kundi.
Post a Comment