Xi
Jinping amethibitishwa rasmi kuwa mtu ambaye ataiongoza Uchina katika kipindi
cha miaka kumi ijayo.
Bwana Xi, aliongoza
mkutano wa kamati kuu ya chama cha Kikomunisti nchini Uchina maarufu kama
Politburo uliofanyika katika ukumbi wa baraja la mji mkuu wa nchi hiyo Beijing,
hatua inayoashiria kupandishwa kwake kuwa kiongozi wa chama hicho
tawala.
Akiongea wakati wa
mkutano huo Bwana Xi alisema kuwa, chama hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi
lakini atafanya kazi ili kuhakikisha kuwa ameafikia matakwa na matarajio ya raia
wa nchi hiyo.
Wengi wa viongozi wapya
katika kamati hiyo wanaonekana kuwa wanasiasa wahafidina na wale waliokisiwa
huenda wakaleta mabadiliko hawakupandishwa cheo.
Xi Jinping anachukua
mahala pa Hu Jintao, ambaye chini ya utawala wake, uchumi wa Uchina umekuwa kwa
kiasi kikubwa.
Hatua hiyo sasa
imekalisha shughuli rasmi ya kukabithi madaraka ya nchi kwa kizazi
kipya.
Baada ya mkutano huo
kukamilika, Bwana Xi, aliondoka kwenye ukumbi huo akifuatwa na Bwana Li Keqiang,
ambaye atamrithi Waziri mkuu wa nchi hiyo Wen Jiabao, na wanachama wengine
watano wenye ushawishi mkubwa katika kamati hiyo kuu ya chama, ambayo awali
ilikuwa na wanachama Tisa lakini imepunguzwa hadi wanachama
Saba.
Watano hao ni pamoja na
makama wa rais, Zhang Dejiang, kiongozi wa chama hicho mjini Shangai, Yu
Zhengsheng, afisa mkuu anayehusika na masuala ya habari na propaganda Liu
Yushan, Naibu Waziri Mkuu
Wang Qishan na kiongozi wa chama cha Tianjin Zhang Gaoli.
Wang Qishan na kiongozi wa chama cha Tianjin Zhang Gaoli.
Viongozi hao wana
majukumu makubwa na Bwana Xi, amesema dhamira yao kuu ni kuunganisha na kuongoza
chama hicho na kuifanya taifa hilo kuwa thabiti na lenye ushawishi
zaidi.
Post a Comment