SERIKALI imesema zimebaki siku
11 kabla ya kuanza kuwakamata watumishi wote wanaotumia namba za kiraia kwenye
magari yake,kinyume cha sheria na utaratibuAkizungumza na wandishi wa habari
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Injinia John Ndunguru, alisema serikali iliweka utaratibu unaozuia matumizi ya
namba za kiraia kwenye magari yake isipokuwa kwa kibali maalum kutokana na
kubaini kuwa, kupitia namba hizo, magari ya Umma yalikuwa yakitumiwa vibaya na
baadhi kupotea.
Alisema Oktoba 19 mwaka
huu waziri wa wizara hiyo, John Magufuli alitoa agizo kuwa hadi Novemba 15 mwaka
huu itakuwa siku ya mwisho ya kusajiliwa magari yote ya Umma kulingana na
sheria na taratibu za nchi.
Akifafanua, Ndunguru
alisema magari yote ya Umma katika wizara, Idara za serikali na taasisi za Umma
yanayotumia nambaza kiraia, magari hayo yanapaswa kusajiliwa kwa utaratibu
uliowekwa na Serikali ambao unataka magari yote ya Umma kuwa na namba zifuatazo,
magari ya Serikali Kuu yatakuwa na mamba za ST, Serikali za Mitaa namba za SM,
Mashirika ya Umma namba za SU na yale yaliyotolewa na Washirika wa Maendeleo kwa
ajili ya miradi wanayoisaidia, namba za DFP.
Mengine ni yale ya vyombo
maalum kama Jeshi (JW), Polisi (PT), na Magereza ambao wataanza kutumia namba
mpya za MT.
Ndunguru alisema baada ya
agizo serikali itaendesha msakao mkali wa kukamata magari ambayo yatakuwa bado
hayajasajiliwa kwa namba za serikali.
“Sheria ya usalama
barabarani ya mwaka 1973 kifungu Na. 30 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004
inaipa wizara ya ujenzi kusajili na kutunza kumbukumbu za magari yote ya
Serikali ambayo yatapewa namba zitakazotanguliwa na JW, PT, ST (sheria na 62),
na DFP (GN. No.517 ya Novemba 29, 2002”alifafanua
Ndunguru.
Ndunguru
aliwatahadharisha wote ambao wana magari ya Umma, ambayo bado yanatumia namba za
kiraia kubadili usajili huo, haraka ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kinidhamu
na kisheria kwa kufikishwa mahakani kwa makosa ya jinai.
Post a Comment