Mwalimu wa Shule ya Msingi Kwamwachalima, iliyopo katika
Kijiji cha Kwamwachalima Kata ya Komkonga wilayani Handeni Mkoa wa Tanga,
ametoweka baada ya kutuhumiwa kufanya mauaji ya kinyama kwa mwanafunzi wa darasa
la tatu na kumjeruhi vibaya mwingine wa kidato cha pili.
Mwalimu huyo, Suhalungi Nangoma (23)
anatafutwa na Polisi kwa tuhuma hizo za
kuua na kujeruhi kwa kisu wanafunzi hao ambao ni ndugu, na watoto wa mwalimu
mwenzake, Ijumaa Mjaliwa.
Nangoma anatuhumiwa kumuua kwa kumchoma kisu kifuani binti huyo anayesoma darasa la tatu katika shule hiyo, Farihia Mjaliwa (9), kisha kumjeruhi kwa kumcharanga kisu tumboni kaka wa binti huyo, Mohamed Farhia anayesoma kidato cha pili katika Sekondari Kisaza.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,
Jafari Mohamed alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wanaendelea
kumsaka mtuhumiwa ili afikishwe mahakamani.
Taarifa zilizopatikana kutoka katika eneo la
tukio na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu zilieleza
kuwa tukio hilo lilitokea saa 9:00 usiku Novemba 23, mwaka huu wakati mtuhumiwa
alipowavamia watoto hao chumbani kwao na kuanza kuwashambulia kwa
kisu.
Baba mzazi wa watoto hao, Mjaliwa anafundisha shule moja ya Kwamwachalima anasema hawakuwahi kugombana.
Baba mzazi wa watoto hao, Mjaliwa anafundisha shule moja ya Kwamwachalima anasema hawakuwahi kugombana.
Mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo huku
akikabiliwa kesi ya kumpachika mimba mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule
ya Sekondari ya Kisaza.
Akisimulia mkasa uliowakuta watoto wake
mbele ya mkuu wa wilaya, Mjaliwa alisema Mohamed ambaye alinusurika kifo,
alichomwa kisu tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje na kwamba sasa amelazwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga.
Kwa mujibu wa Mjaliwa, mtuhumiwa baada ya kufanya kitendo hicho alimgeukia mdogo mtu na kisha kumchoma kisu kifuani upande wa kushoto na kukiacha kikining’inia.
“Watoto hao walianza kupiga kelele kutoka na mashambulizi hayo, lakini mtuhumiwa alitimua mbio na kukimbilia kusikojulikana,” alisema Mjaliwa ambaye hakuwepo siku ya tukio.

“Cha kushangaza alikuwa nje kwa dhamana kwa
kumpa mimba mwanafunzi,” alisema.
Habari zinadai kuwa siku ya tukio, baadhi ya walimu wa Shule ya Kwamwachalima walifanya kikao kifupi kujadili jinsi ya kumwekea dhamana Nangoma, iwapo angefikishwa mahakamani kwa kesi ya kumpachika mwanafunzi mimba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Ali
Hatibu, alisema walimhoji majeruhi huyo kabla hajapoteza fahamu na kumtaja
mwalimu huyo kwamba ndiye aliyemchoma kisu.
“Tuliingia chumbani kwa watoto na kukuta
kumetapakaa damu nyingi, lakini binti huyu ambaye sasa ni marehemu tulikuta
tayari ameshafariki dunia na alikuwa ameshikilia kisu, maana alichomwa kwenye
moyo,” alisema Hatibu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kwamwachalima, Eva
Msenga alisema kwamba siku ya tukio mchana alizungumza na mtuhumiwa baada ya
kuona mwenendo wake hauridhishi na kwamba alimjibu kwamba alikuwa
amechanganyikiwa kutokana na kesi inayomkabili.
Msenga alisema baadaye jioni alikuwa na
watoto hao wakijisomea hadi saa tatu usiku, na kwamba muda huo aliwataka
wakalale kwani muda ulikuwa umekwenda.
“Tuliagana na waliondoka kwenda kulala,
baadaye usiku ndipo tuliposikia tukio hili na tuliambiwa kwamba mtuhumiwa
alibisha hodi na watoto kwa kumfahamu walimfungulia kisha akawafanyia unyama huo
wa kutisha,” alisimulia Msenga.
Post a Comment