|
Katibu
wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesahihisha taarifa alizotoa jana kuhusu uteuzi wa
Meneja mpya wa timu na Ofisa Habari. Mwalusako amesema Shaaban Katwila
aliyemtaja jana kuajiriwa kama Meneja mpya wa timu na Bakari Kizuguto aliyetajwa
kuwa Ofisa Habari, kwa usahihi wameomba tu kazi, lakini hawajapitishwa katika
ajira bado. Mwalusako ameomba radhi wapenzi wa soka, hususan wanachama na
mashabiki wa Yanga kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hizo.
Amesema mchakato wa kuwapata Maofisa wapya wa kushika nyadhifa hizo bado
unaendelea.
Pichani
ni Mwalusako (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu,
makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam leo kusahihisha
taarifa yake ya jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa klabu
hiyo. |
on Tuesday, November 6, 2012
Post a Comment