Na
Elizabeth John
BAADA ya kukaa kimya kwa muda
mrefu, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini Ali Kiba baada ya kukaa kimya kwa
muda mrefu ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘My
everything’.
Akizungumza na Habari Mseto
jijini Dar es Salaam, Alikiba amesema alikuwa kimya kwa muda mrefu sasa
amejipanga na ameamua hivyo mashabiki wakae tayari kupokea burudani kutoka
kwake.
“Nilikuwa kimya kwa muda
mrefu sasa nimejipanga na nimeamua kutoa burudani kwa mashabiki wangu hivyo
watarajie vitu vizuri mfurulizo kutoka kwangu,” amesema
Alikiba.
Amesema sasa anatarajia kutoa
vitu mfululizo kwaajili ya kuwapa burudani mashabiki wake na kudai kuwa baada ya
wiki mbili mbele atakuwa ameanza kusambaza video ya kibao
hicho.
“Kkwasasa ukichelewesha kutoa
video wimbo unachuja haraka hivyo [sipo tayari kuaribu kazi yangu nimejipanga na
nimeamua ntaakikisha video inatoka mapema kabla ya kibao hicho kuchuja,” amesema
Alikiba.
Post a Comment