Athumani Nyamlani |
Na Princess
Asia
MAKAMU wa
Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani
ameteuliwa kuwemo kwenye Ujumbe rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
utakaosimamia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika
Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba,
uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na Kamati yake ya Utendaji.
Ujumbe huo wa CAF kwa ajili ya fainali hizo zitakazoanza Januari 19 na
kumalizika Februari 10 mwaka huu una jumla ya watu
148.
Wambura
amesema Nyamlani atakuwa miongoni mwa wajumbe watatu, watakaoshughulikia masuala
ya rufaa kwenye mashindano hayo. Wajumbe wengine ni Prosper Abega kutoka
Cameroon na Pierre-Alain Monguengui wa Gabon. Nyamlani ni mjumbe wa Bodi ya
Rufani ya CAF yenye watu 12.
Post a Comment