Rais Barack Obama ameibuka na ushindi baada ya kupata kura za majimbo 303 kati ya 206 zake Romney. Ushindi wa Obama umevuka malengo kwani ili awe Rais alihitajika kupata kura za majimbo 270 ila yeye (Obama) amepata kura za Majimbo 303
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Post a Comment