Aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Urusi Anatoly
Serdyukov kataka
midotcomnewsindonesia.wordpress.com.
Putin
ameziba pengo la waziri Anatoly Serdyukov ambaye amekuwa akitekeleza mageuzi ya
kijeshi yasiyo maarufu ingawa yaliungwa mkono na chama cha Kemlin kwa kumpa
nafasi hiyo gavana wa zamani wa jimbo la Moscow na waziri wa mambo ya dharura
Sergei Shoigu.
Wachambuzi
wanasema kwamba kufutwa kazi kwa afisa huyo wa juu ambaye amenufaika na uungwaji
mkono usio na masharti wa rais Putin ni hatua inayolenga kuwatia hofu wasomi
wakati rais huyo anapo pambana na mgogoro mbaya wa kisiasa katika miaka takriban
13 ya uongozi wake.
Putin
aamesema kuwa Serdyukov, mmoja wa watu watatu nchini Urusi wenye uwezo wa kupata
namba ya kianzio ya uzinduzi wa nyuklia, ameondolewa katika wadhifa wake ili
kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa ya dola.
Post a Comment