Philemon Ntahilaja |
MDAU wa soka
nchini, Philemon Ntahilaja, mgombea nafasi ya Uwakilishi wa Klabu katika
Uchaguzi wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), amesema kwamba anaamini kwa
uzoefu na uelewa wake mkubwa katika mchezo wa soka kwa ujumla, akipata nafasi
hiyo atasaidia maendeleo ya klabu Dar es Salaam.
Baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi
hiyo, Ntahilaja alisema kwamba ameamua kwa makusudi sasa kujitolea kusaidia
maendeleo ya soka Dar es Salaam, kwa kuwa ana uwezo wa
kutosha.
“Nimekuwa
mchezaji wakati nipo shule, nimekuwa kiongozi kwa muda mrefu katika Kamati
mbalimbali za Kitaifa na klabu kubwa pia kama Yanga, lakini kikubwa ni mpenzi wa
soka, nimejifunza mengi na sasa ni wakati mwafaka kwangu kuwatumikia wana Dar es
Salaam,”alisema Ntahilaja.
Ntahilaja
ndiye Mwenyekiti wa kwanza na mwasisi wa kundi la Yanga Family, ambalo lina
matawi hadi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Kwa sasa pia
ni Mjumbe wa kamati ya Masoko na Matangazo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Saidia Taifa
Stars.
Lakini pia
Ntahilaja amekuwa ndani ya Kamati za Yanga tangu mwaka 1998 na amekuwa na
mchango mkubwa kutokana na desturi yake ya kupenda kujitolea kwa hali na mali.
Post a Comment