MWENYEKITI wa klabu ya
Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kwamba uongozi umebaini
kwamba wengi wa wanachama wa tawi la Mpira Pesa waliojiorodhesha ili kushinikiza
kufanyika kwa mkutano wa dharura wa klabuu hiyo si hao.
Hatua hiyo inafuatia
wanachama hao kufanya maadhimio ya kujiorodhesha ili kufikisha akidi
itakayotimiza mashaerti ya kufanyika kwa mkutano ili kuwaonmdoa madarakani
viongozi wa sasa kwa madai ya kushindwa kuongoza.
Rage amesema pamoja na
kubaini hilo ,
pia uongozi umegundua kwamba majina ya wanachama hao yamenakiliwa katika leja
ya wanachama ambayo ilipotea mikononi mwa kiongozi mmoja wa
zamani.
Alisema uongozi
unaheshimu jitihada zinazofanywa na wanachama hao na kuzifanyia kazi, lakini
hauwezi kutekeleza vitu ambavyo havikidhi vigezo vilivyopo katika katiba ya
klabu hiyo.
Rage alisema, katiba ya
sasa ya Simba haiwatambui wanachama waliopo kwenye leja, badala yake inawatambua
wale waliosajiliwa katika kompyuta.
“Pamoja na wanachama
hao kunakiliwa katika leja,tumebaini hata saini zilizowekwa ni za kughushi na
tukifanya uchunguzi hasa tutabaini ni wengi tu hawana sifa, kitu ambacho
kinakwenda kinyume na katiba ya Simba,”alisema Rage
Rage aliongeza kuwa,
wanaamini mchakato huo unafanywa na baadhi ya watu wanaotaka kuleta chokochoko
ndani ya klabu hiyo kitu ambacho ni kigumu kukitimiza kwa vile uongozi upo imara
na unafuata katiba ya klabu hiyo.
“Hatuwezi kujiuzuilu
kwa ajili ya shinikizo la watu ambao tunafahamu wanatumika, sisi tunaongoza kwa
kufuata katiba na tutachukua uamuzi kwa mujibu wa katiba pindi
inapostahili,”alisema
Aidha, Rage aliongeza
kwamba uongozi wa klabu hiyo ulitarajiwa kukutana jioni ya jana kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mzunguko
wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika wiki iliyopita na Simba kushika
nafasi ya tatu.
Hivi karibuni baadhi ya
wanachama waliutakla uongozsi wa Simba chini ya Rage kuachia ngazi baada ya timu
hiyo ambayo ilikuwa ikiongoza ligi kwa kipindi kirefu kupoteza mwelekeo baada ya
kupoteza michezo yake.
Post a Comment