Rais Felipe Calderon wa Mexico ametuma mswada katika bunge la Congress akitaka kubadilishwa kwa jina rasmi la nchi hiyo.
Jila la sasa la ‘United States of Mexico’ liliasiliwa mwaka 1824 na lilikuwa na lengo la kuiga majirani zao wa kaskazini.
Rais Calderon anataka libadilishwe na kuwa ‘Mexico’ kama linavyo fahamika duniani kote.
Calderon anayeondoka madarakani Disemba Mosi mwaka huu, amesema Mexico haihitaji tena kuiga nguvu yeyote ya kigeni.