Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein kesho anatarajiwa
kufunguwa Mkutano wa 34 wa Juimuia ya kiafrika ya Utumishi wa Umma na
Uongozi(AAPAM) huko Zanzibar Beach Resort nje kidogo wa Mji wa
Zanzibar.
Kwa mujibu wa Ratiba
iliotolewa na Jumuia hiyo imeonesha kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi DKT Abdulhamid Yahya Mzee atatowa maelezo juu ya Mkutano
huo.
Baadae Rais wa AAPAM Abdon
Agaw Jok Nhial nae atatowa maelezo juu ya Mkutano huo kwa upande wa Jumuia
hiyo ambapo pia Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Celina Kombani atatowa Maelezo na
baadae kumkaribisha Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ambae atahutubia Mkutano
huo.
Wajumbe kadhaa wa Mkutano
huo tayari wameshawasili Zanzibar akiwamo Katibu Mkuu wa AAPAM
.
Jumla ya Wajumbe 500
wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano huo ambapo mwaka jana Mkutano kama huo
ulifanyika Nchini Malawi.
Mbali na Mkutano huo
Wajumbe hao pia watapata fursa yakutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya
Utalii viliopo Zanzibar pamoja na kutembelea Mji Mkonge na sehemu za
Historia.
Mkutano Huo wa AAPAM wa
siku tano unatarajiwa kumalizika tarehe
16/11/2012
Post a Comment