MKURUGENZI Mkuu
wa Shirika la Habari, BBC, George Entwistle amejiuzulu wadhifa huo. George
Entwistle amejiuzulu kama Mkurugenzi BBC kwa kile kufanyika makosa katika moja
ya vipindi vya shirika hilo la habari Ulimwenguni. Taarifa zaidi zinasema
Entwistle amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa
iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.
Taarifa hiyo kwa makosa
ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative, Lord
McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto. Tayari shirika
la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa
zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.
Kipindi hicho cha
Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchunguzi kuhusiana
na kashfa ya Bwana Savile. Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi, usiku
Entwistle alisema; “ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu
kulifanya”.
Akisimama kando yake
Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema; “huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa
majozi katika maisha yangu ya umma”. “Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo
cha habari kinachoaminika”
“Kama Mhariri Mkuu wa
shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amediriki kujiuzulu kutokana na
makosa yasiokubalika – uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko
mengi”.
Post a Comment