MAKUNDI ya upinzani nchini
Syria yanayokutana mjini Doha, yamekubaliana kimsingi kuhusu mpango wa umoja
dhidi ya rais Bashar al-Assad.
Washiriki wa mkutano huo
wamesema ambapo watakutana leo.
"Tumekubaliana kuhusu
vipengee viwili juu ya kuundwa kwa muungano wa kitaifa nchini Syria kwa ajili ya
majeshi ya upinzani na mapinduzi.
Tutaendelea na majadiliano
yetu kuhusu mambo yanayohusika katika muungano huo leo Jumapili," mmoja wa
viongozi wa muungano huo wa upinzani Suhair Atassi ameliambia shirika la habari
la AFP baada ya saa 12 za mazungumzo.
Kiongozi mpya wa SNC George
Sabra.
"Tulikuwa katika hatua ya
kutia saini makubaliano lakini tumeonelea kutoa muda zaidi ili kutathmini sheria
za ndani kwa ombi la baadhi ya makundi," amesema mjumbe mwingine Riad Seif,
ambaye anaripotiwa kuwa anaonekana na serikali ya Marekani kuwa ana uwezekano wa
kuwa mkuu mpya wa upinzani.
NSC lakabiliwa na
mbinyo.
Washiriki walitarajiwa
kurejea katika mazungumzo leo asubuhi. Mkutano huu unakuja baada ya baraza la
taifa la Syria SNC kukabiliwa na mbinyo kutoka kwa mataifa ya Kiarabu na mataifa
ya magharibi kukubali mpango wa umoja wa upinzani, huku kukiwa na hali ya kukata
tamaa miongoni mwa makundi ya wapiganaji.
Hapo nyuma likiwa
linatambulika kama wawakilishi wakuu wa upinzani lakini kadiri ya muda
ulivyokwenda lilipoteza hadhi hiyo katika serikali ya Marekani , kutokana na
kudhibitiwa na watu ambao wanaishi uhamishoni na hawana uhusiano wa karibu na
hali halisi ndani ya nchi, baraza hilo la SNC , lilitakiwa mara mbili kuahirisha
mazungumzo juu ya mpango wa kuunda serikali itakayojumuisha makundi mengi ambayo
itakuwa inasubiri kuchukua madaraka ndani ya Syria.
Makubaliano hayo yako
katika msingi wa harakati zinazochukuliwa na Seif ambazo zina lenga kuundwa kwa
serikali ya mpito , ambalo ni baraza la kijeshi litakaloshughulikia makundi ya
waasi ndani ya Syria na mahakama ambayo itafanyakazi katika maeneo
yanayoshikiliwa na waasi.
Mjumbe muhimu wa mkutano wa
Syria mjini Doha Riad Seif
Serikali ya
mpito
Serikali ya mpito ambayo
itakuwa na wajumbe kumi itachaguliwa na kundi jipya lenye wajumbe 60 ambalo
litatokana na wanaharakati wa kiraia na wapiganaji waasi ndani ya Syria, pamoja
na wale wanaoishi uhamishoni ambao wamedhibiti baraza la SNC.
Jana Jumamosi (10.11.2012)
baraza la NSC limewasilisha pendekezo lake na kiongozi wake mpya George Sabra
amewaambia waandishi habari mjini Doha kuwa baraza hilo la NSC ni la muda mrefu
zaidi kuliko harakati nyingine zozote, akiongeza kuwa makundi ya upinzani
hayapaswi kulazimishwa kuwa chini ya chombo chochote kingine.
Rais wa Syria Bashar
al-Assad.
Kwa mujibu wa shirika
linaloangalia haki za binadamu nchini Syria , zaidi ya watu 37,000 wameuwawa
tangu vuguvugu la harakati za kuuondoa utawala wa rais Bashar al-Assad kuzuka
Machi 2011, harakati hizo zilipoanza kwanza kama vuguvugu la amaandamano na
kisha kugeuka uasi wa mapambano ya silaha.
Post a Comment