Snoop Lion (dogg
Rapper mkongwe aliyejulikana kwa jina la
Snoop Dogg kabla hajabadilisha na kuwa Snoop Lion, mwaka huu baada ya kuhamia
kwenye muziki wa reggae na kulazimika kuchill Jamaica ili kukamilisha project
yake ya album ya reggae, ameamua kujiunga na jamii ya Jamaica pia katika
kusaidia kusolve tatizo la ukosefu wa chakula na matunda hasa kwa watoto.
Snoop Lion ametangaza kuwa na ushirika
na Reed’s Ginger Brew ili kusaidia mradi unaoitwa Mind Gardens
Project.
Project yake hii ambayo haipo kwa ajili
ya kuingiza faida (non profit) , ina lengo la kuhakikisha inatengeneza bustani
endelevu za jamii. Bustani hizo zitatoa matunda ya asili na mboga kwa ajili ya
watoto nchini Jamaica.
Snoop mwenyewe aliandika statement,
“nilipoenda Jamaica, tulichukua muda kwenda kutembelea hizi jamii huko Kingston,
na niliadhiriwa sana na umasikini na ukosefu wa chakula bora kwa watoto.”
Snoop aliendelea kudondosha maandishi
kwa feeling za alichokiona na kutoa ahadi, “hakuna mtoto atakaepata njaa. Baada
ya inspiration niliyoipata kutoka Jamaica, najisikia msukumo wa kuchukua jukumu
kutengeneza kitu ili kuirudishia jamii.”
Project hii imeshaanza tayari huko
Kingston na imeshazifaidisha jamii mbili kubwa , Trench Town na Tivoli Gardens.
Post a Comment