Paroko wa Parokia ya
Isimani, Baba Anjelo Burgo akiwa kitandani kwenye chumba maalumu katika
Hosptali ya Mkoa wa Iringa wakti akisubiri kufanyiwa upasuaji kwa lengo la kutoa
risasi zilizosalia mwilini baada ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa
na silaha za jadi na Bunduki kuvamia nyumba wanazoishi mapadri usiku wa kuamukia
jana. Picha na Said Ng’amilo.
MAPADRI wawili wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Isimani, Jimbo la Iringa, wamejeruhiwa vibaya na kulazwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kutokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi kuwajeruhi kwa silaha za jadi na bunduki, baada ya kuvamia nyumba
wanazoishi.
Paroko wa Kanisa hilo
Angelo Burgio kutoka Italia (60) na msaidizi wake Herman Myala walikumbwa na
mkasa huo usiku wa kuamkia jana.
Padri Burgio alijeruhiwa
kwa kupigwa risasi mbili kifuani na kucharangwa mapanga, msaidizi wake Padri
Myala alijeruhiwa kwa mapanga na kuburutwa chini kwenye ardhi.
Tukio hilo limetokea
ikiwa ni siku moja tangu kuvamiwa kwa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa lililopo
eneo la Kihesa mkoani humo, ambapo mlinzi wa kanisa hilo, Batholomea Nzigilwa
(65) alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Nzigilwa amelazwa katika
Hospitali ya Mkoa wa Iringa, huku hali yake ikielezwa ikiwa ni
mbaya.
Watangaza
msamaha.
Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Akizungumza kwa tabu,
padri huyo alisema majambazi hao walifika eneo la Kanisa la Kihesa saa tano
usiku wakiwa na silaha mbalimbali za jadi na bunduki.
Alisema baada ya
kumshambulia msaidizi wake, walimfyatulia yeye risasi kifuani wakati alipofungua
mlango na kutaka kukimbia.
“Mimi baada ya kuwasikia
nilifungua mlango kwa lengo la kutaka kukimbia ili nijinusuru, lakini hamadi
wakanifyatulia risasi kifuani.
Nilianguka chini na
walipoingia ndani walichukua fedha taslimu Sh3.5 milioni zilizokuwa chumbani
kwangu na kisha kunikata na panga kichwani, ” alisema Burgio.
Hata hivyo, padri huyo
alisema, “Sisi tunawasamehe. Mimi na mwenzangu tumewasamehe tangu walipofanikiwa
kutushambulia na kukimbia. Tunawaombea msamaha kwa Mungu kwani yeye ndiye
anayejua,” alisema Padri Burgio.
Post a Comment