RIPOTI YA NCHI MASIKINI
SANA DUNIANI MWAKA 2012
UKWELI WA MAMBO NA
TARAKIMU
Geneva,
26 Novemba 2012 – Ripoti ya Nchi Maskini Sana Duniani
ya Mwaka 20121, yenye kichwa kidogo cha habari Kutumia Fedha
Zinazotumwa na Raia Wanaoishi Nga’ambo na Weledi Wao Kujenga Uwezo wa
Uzalishaji, imetolewa leo.
Mwelekeo wa
uhamiaji
Ø Idadi ya watu ambao wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs)
iliongezeka kutoka milioni 19 mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka
2010. Hii ni sawa na 3.3% ya
wakazi wote wa nchi hizo.
Ø Nchi Maskini Sana Duniani zinatoa 13% ya wahamiaji duniani
kote---idadi ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi ya wakazi wote
duniani (12.1%).
Ø Wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi
zinazoendelea (Kusini) na mmoja tu kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi
zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji
fedha
Ø Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye
nchi zao kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni
3.5 kufikia dola bilioni 27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha kimeendelea
kuongezeka pamoja na kuwepo na anguko la kiuchumi
duniani.
Ø Mwaka 2011 kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka
Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada dola milioni 3.2 na kutoka
Kenya dola milioni 2.5.
Ø Mwaka 2011, fedha zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya
thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15),
na kiwango hiki kilizidiwa tu na Misaada Rasmi Kutoka Nje, yaani ODA (dola
bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha fedha kutoka nje ya
nchi.
Ø Kiwango cha fedha zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa
mwananchi mmoja mmoja kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi
dola 30 kati ya mwaka 2000 na 2010.
Ø Fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs
ikilinganishwa na nchi zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha
zinazotumwa na raia kutoka nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na 15% ya
thamani ya bidhaa zinazouzwa nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa mara tatu
ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea (ambazo siyo
LDCs).
Ø Kuanzia mwaka 2008 hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka
nga’mbo kinalingana na zaidi ya moja ya tano ya pato la taifa la nchi za
Lesotho, Samoa, Haiti na Nepal.
Ø Tangu mwaka 2009 hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi
za nje kutoka kwa raia wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi zilipata
kutokana na mauzo ya bidhaa nje.
Ø Kwa LDCs tisa, kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje
kilizidi kile cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi
kutoka nje (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi ni nchi za Bangladesh, Haiti, Lesotho,
Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na Yemen. Kwenye nchi nyingine nane za kundi
la LDCs, katika kipindi hicho hicho, fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo
zilizidi FDI: Benin, Burundi, Comoros, Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati
na Uganda.
Ø Theluthi mbili ya fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo kwenda
kwenye LDCs zinatoka kwenye nchi zinazoendelea.
Ø Duniani kote, gharama ya kutuma fedha zinafikia 9% ya kiwango cha
fedha kilichotumwa; kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi kwa theluthi moja
(12%).
Ø Kama nchi zilizo kusini kwa Jangwa la Sahara zingelipia gharama za
uhamishaji fedha kwa wastani wa gharama inayolipwa duniani kote, mapato yao
yangekuwa yaliongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka 2010.
Ø Asilimia 66 ya fedha zilizohamishwa kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka
2009 na 2011 ni za nchi tatu tu: Bangladesh, Nepal na
Sudan.
Ø Matumizi ya simu za mkono kwenye LDCs ni makubwa zaidi (368 kwa kila
wakazi 1,000) kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa wakazi 1,000). Simu za
mkono zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na kupokea fedha kutoka
ng’ambo.
Kuhama kwa
utaalam
Ø Mtu mmoja kati ya kila watu watatu wenye ujuzi mkubwa (mwenye elimu ya
chuo kikuu) kutoka LDCs anaishi ng’ambo. Kwenye nchi zilizoendelea kiwango ni mtu mmoja katika kila watu
25.
Ø LDCs sita zina raia wao wataalaum wengi zaidi wanaoishi nje ya nchi
kuliko wale waliobakia nchini mwao: Haiti, Samoa, Gambia, Tuvalu na Sierra
Leone.
Ø Theluthi mbili ya wahamiaji wenye ujuzi mkubwa kutoka LDCs wanaishi
kwenye nchi zilizoendelea; theluthi moja wanaishi katika nchi
zinazoendelea.
Ø Kiwango cha kuhama kwa watu wenye ujuzi kwenda ng’ambo ni kikubwa
(20% ) kwa LDCs nyingi (30 kati ya 48).
Ø Wahamiaji kutoka LDCs wenye elimu ya chuo kikuu ambao wanaishi na
kufanya kazi ng’ambo inafikia milioni 2.
Ø Idadi ya Watanzania waliohamia Uingereza kwa kumbukumbu za mwaka 2000
ni 10,535.
Ø Aina ya wahamiaji inafuata ukubwa wa kipato wa nchi mwenyeji. Katika
nchi zilizoendelea, 35% ya wahamiaji ni wale wenye elimu ya chuo kikuu; kwenye
LDCs 4% tu ya wahamiaji wana kiwango hicho cha elimu. Viwango hivi ni kwa
wahamiaji kutoka nchi zote, japo viwango ni hivi hivi kwa wahamiaji kutoka nchi
za kundi la LDCs.
Ø Theluthi moja ya wahamiaji kutoka LDCs ambao wana elimu ya chuo kikuu
wanaishi Marekani.
Uwezo wa kiuchumi
(Uchumi mpana)
Ø Kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka kwa LDCs tangu kipindi cha
msukosuko wa kiuchumi duniani (2009-2011) ni 4.7%, ambacho ni chini ya kiwango
cha kipindi cha miaka ya ukuaji mkubwa wa kiuchumi (2003-2008), yaani 7.9%. Hii
ina maana kwamba kiwango cha ukuaji wa kipato kwa mwaka kwa kila mkazi kilishuka
kutoka 5.4% miaka ya ukuaji mzuri wa uchumi hadi kufikia
2.4%.
Ø Wastani wa ukuaji halisi wa pato la nchi katika LDCs mwaka 2011, yaani
4.2%, ulikuwa chini ya 4.9% ya mwaka 2009 wakati wa anguko la uchumi
duniani.
Ø Kile kinachojulikana kama Gross fixed capital formation kwenye
LDCs kilipanda kidogo kutoka 20.7% ya pato la jumla la taifa mwaka katika miaka
ya 2005-2007 kufikia 21.6% miaka ya 2008-2010. Hata hivyo, bado kilibaki chini
ya viwango vya nchi nyingine zinazoendelea, ambazo zilifikia kiwango cha
30.1%.
Ø LDCs zinaendelea kutegemea sana raslimali kutoka nje. Pengo la pato
linalotokana na uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa nje lilikuwa kubwa kwa 20% ya
pato la jumla la taifa katika nchi tano za kundi la LDCs mwaka 2011, wakati LDCs
nyingine 13 pengo lilikuwa asilimia 10 ya pato la jumla la
taifa.
Ø Kiwango cha utegemezi wa rasilimali kutoka nje katika kulipia
uwekezaji wa ndani ya nchi kati ya mwaka 2008 na 2010 kilikuwa 15% ya pato la
jumla la taifa kwa LDCs ambazo hazisafirishi mafuta
nje.
Ø Asilimia 62 ya mauzo ya bidhaa nje kutoka LDCs 48 yalikuwa ni kutoka
nchi tano tu: Angola, Bangladesh, Equatorial Guinea, Yemen na Sudan. Ukiacha
Bangladesh, nchi zote hizi zinauza mafuta nje.
Ø Mapato ya LDC kwa mauzo ya bidhaa nje yanategemea zaidi mauzo ya
bidhaa moja (mafuta), ambayo yanaingiza 46% ya jumla ya mapato yote yanayotokana
na mauzo ya bidhaa nje.
Ø Zaidi ya nusu ya mauzo ya nje kutoka LDCs (54%) yalikuwa yanakwenda
kwenye nchi zinazoendelea mwaka 2011, mwelekeo unaothibitisha umuhimu wa
biashara ya kusini-kusini. China ndiyo iliyonunua bidhaa nyingi zaidi kutoka
LDCs (26.4%) ikiwazidi Jumuia ya Ulaya (20.4%) na Marekani
(19%).
ZIKO WAPI NCHI MASKINI
SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa
unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo wao
ni kama ifuatavyo.
Africa
(33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic,
Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC), Djibouti, Equatorial
Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia,
Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na
Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Zambia;
Asia
(9): Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal,
Timor-Leste na Yemen;
Caribbean
(1): Haiti;
Pacific (5):Kiribati,
Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu.
Kutengeneza list ya
LDCs
List ya LDCs inapitiwa
upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) la Umoja
wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya kamati ya Sera ya Maendeleo
(CDP).
Katika mapitio ya hivi
karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo
vifuatavyo:
1. Kigezo cha pato la kila mtu, kwa kufuata Pato la Jumla la Nchi (GNI)
kwa kila kichwa (wastani wa miaka mitatu)
2. Kigezo cha raslimali watu ambacho kinatumia viashiria kama lishe,
afya, kuandikishwa shuleni na kujua kusoma na
kuandika
3. Kigezo cha mazingira hatarishi ya kiuchumi. Ambacho kinatumia
viashiria kama mishtuko ya kiasili, mishtuko ya kibiashara, udogo na
umbali.
Nchi tatu tu
zimefanikiwa kupanda daraja kutoka list ya nchi za kundi la LDCs: Botswana
Desemba 1994, Cape Verde Desemba 2007 na Maldivs Januari 2011. Samoa
inategemewa kupanda daraja tarehe 1 Januari 2014.
ECOSOC ilipitisha
pendekezo la CDP kuipandisha daraja Equatiorial Guiones mwezi Julai mwaka 2009
na mwezi Julai 2012 ikakubali pendekezo la CDP kuipandisha Vanuatu. Hata hivyo
ruhusa ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa bado itahitajika ili kuzipandisha
daraja nchi hizi mbili.
Post a Comment